MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Felista King'ung'e (23) mkazi wa Semtema Kihesa,Iringa nusura apoteze maisha yake naya mtoto wake baada ya kukosa huduma ya uzazi katika kituo cha afya cha Ngome, kilichopo ndani ya manispaa ya mji wa Iringa.
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wagonjwa na mashahidio waliokuwepo katika sakata hilo, walisema kwa zaidi ya masaa matatu kituo hicho kilikosa wahudumu, huku kukiwa na mrundikano wa wagonjwa wanaosubiri msaada wa huduma ya afya.
Walisema baada ya kufika mama huyo mjamzito akiwa anaumwa uchungu hakuwepo kituo pia kilikuwa hakina muhudumu wa aina yoyote na hivyo kuwepo hatarini maisha ya mama huyo mjamzito.
Richard Nyaluke alisema, mama huyo mjamzito alikaa kwa zaidi ya saa moja bila msaada, huku kituo kikiwa na mlinzi pekee, licha ya wahudumu kupigiwa simu juu ya mama huyo mjamzito anayehitaji msaada wa huduma ya ukunga.
"Sisi wengine tulikuwa na uwezo wa kusubiri, lakini ilikuwa ni vigumu kwa mjamzito aliyekuwa akihitaji huduma ya ukunga, mimi nilimpeleka mtoto wangu alikuwa amepigwa jiwe la jicho na wenzie lakini kwa zaidi ya masaa mawili sikupata huduma yoyote mpaka niliamua kwenda kwenye duka la dwa ili kumpa mtoto atulize maumivu," Alisema Nyaluke.
Walisema wahudumu wa kituo hicho wamekuwa na desturi ya kutotoa huduma chini ya kiwango licha ya kituo hicho kutegemewa na vijiji vilivyo vingi, na kulalamikia tatizo la ukosefu wa dawa licha ya kuliona gari la MSD ( la dawa likishusha dawa).
walisema dawa zinazopatikana katika kituo hicho ni Mseto na panadol pekee na hivyo kulazimika kununua dawa katika maduka ya madaktari ambayo yapo jirani na kityuo hicho, yaliyowekwa kwa makusudi ya kuwakamua wagonjwa.
Waliitaka serikali kufuatilia kwa karibu utendaji wa kazi za wahudumu wa afya kwani baadhi yao wanajisahau na kusababisha vifo visivyo vya lazima vinavyovhangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
Lakini uongozi wa kituo hicho ulipotakiwa kuelezea mkasa huo uligoma kabisa kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo licha ya kuwa baadhi ya watumishi wa kituo hicho walikuwa wakizungumzia vilivyo mkasa huo na hivyo kulazimika kumtafuta kaimu mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Seveline Tarimo ambaye alikiri kuipata taarifa hiyo na kuwa Manispaa imeunda kamati ya watu watatu ili kubaini tatizo hilo.
Naye Linna Maliva afisa muuguzi wa word ya watoto wachanga chumba cha joto alisema hali ya mtoto huyo inaendele vizuri tofauti na alivyopokewa kwani alikuwa na kilo moja na gramu 400 na sasa zimeongezeka gram kumi.
Mwanamke huyo Felista King'ung'e alisema anaendele vizuri na kuwa alianza kuumwa uchungu kabla ya miezi kutimia, na mtoto huyo niwa kwanza na anamshukuru Mungu kwa kupona yeye na mtoto wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment