MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul (Diamond)
amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, au kutakiwa kulipa fidia ya
shilingi elfu 80 kwa kosa la kumpiga mwandishi wa habari Mkoani
Iringa.
Hatua hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili
kukiri kosa mbele ya mahakama yeye na wenzake kwa kuharibu Camera
mbili, Lap top aina ya Accer pamoja na kumshambulia mwanahabari
Frances Godwin tarehe 31 katika uwanja wa samora mjini hapa.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mh.Masua alisema
kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu
kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila
mmoja na huku wakilazimika kumlipa Frances shilingi elfu 30 kila
mmoja.
Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia
adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja
mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo
wamelifanya kwa ghadhabu.
Mheshimiwa Hakimu ninaomba unipunguzie adhabu licha ya kutenda kosa
hilo, kwani nakili kuwa nilipatwa na hasira kama binadamu na kuamua
kuchukua uamuzi wa kufanya hayo, mimi sikukusudia kuja Iringa kufanya
vurugu bali hali hiyo ilikuja baada ya kupata ghadhabu kama walivyo
binadamu wengine,” alisema Diamond.
Hukumu hiyo ambayo imezua maswali mengi kwa wanahabari na wananchi
waliohudhulia mwenendo mzima wa kesi hiyo na kuomba vyombo vya sheria
kutenda haki pasipo kuangalia umaalufu wa mtuhumiwa.
Naye mwanasheria Evaristo Myovela alisema kesi hiyo hakimu ametimiza
wajibu wake, huku akimshauri Frances kukata rufaa ili kuipeleka kesi
hiyo katika Mahakama nyingine kwa kufuata utaratibu wa sheria katika
kuchukua maamuzi hayo.
Wakati wanahabari wakijadili juu ya hukumu ya Diamond na jeuri
aliyoonyesha mahakamani hapo, mara Waziri wa nchi sera na uratibu wa
sheria wa bunge Willium Lukuvi alikatiza katika mahakama hiyo ndipo
wanahabari wakataa kupata mawazo na uelewa zaidi juu ya kilichotokea
mahakamani hapo.
Diamond alilipa fidia hiyo na kuachiwa huru licha ya France
kulalamikia mwenendo wa kesi hiyo na kuamua kupeleka barua mahakamani
ya kuomba nakara ya kesi na 13. ya 2012 kwa ajili ya kukata rufafaa.
Hata hivyo chama cha wanahabari mkoani hapa kilimtaka Diamond kufanya
naye maongezi, na yeye kuahidi kufika katika ofisi za Clabu ya
wanahabari (IPC) kwa mazungumzo, jambo ambalo amelikaidi mwanamuziki
huyo
MWISHO
No comments:
Post a Comment