Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu, akifanya uzinduzi wa hafla ya kukabidhi Usafiri wa Pikipiki 125 kwa Chama cha akiba na mikopo, Vijana Sacco's - ya Vijana wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Bi. Jesca Msambatavangu akitoa ushauri kwa vijana hao, kuacha kubweteka juu ya hatua hiyo ya usafiri wa Pikipiki, ambapo amewataka kuwa na mawazo ya mbele zaidi kwa kujipanga kuwa na magari.
"Pikipiki peke yake hazitoshi, haya chukua na hela hizi shilingi Laki tano zisaidie kuukuza mfuko wa Sacco's yenu vijana, ninawapenda sana vijana wanaojituma, nyinyi kwa mpango huu ni rafiki zangu sana sasa," Alisema Msambatavangu.
Akinamama walionufaika na mkopo huo wakishukuru msaada huo wa fedha kutoka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu.
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mh. Mahamudu Mgimwa akipongeza vijana hao kwa hatua ya kuunganisha nguvu zao na kumuomba awe mdhamini wa wazo la kupata usafiri huo wa Pikipiki, ambapo Mgimwa aliwaasa vijana hao wajitume kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kwani hiyo ndiyo siri ya mafanikio.
Kundi la Vijana Sacco's - Mkoani Iringa wakiwa
katika uwanja wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo mara
baada ya kukabidhiwa Usafiri huo wa Pikipiki.
Mwenyekiti wa Vijana Sacco's Bw. Baraka Frenk akiwasikiliza wanachama wa Sacco's mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki hizo, ambazo zitasaidia kurahisisha usafiri, huku baadhi yao wakitumia kama ni sehemu ya ajira.
Vijana waliopata mkopo wa Pikipiki wakiwasikiliza viongozi waliofika katika hafla hiyo.
"Tupo makini sana"
Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi wakiwa katika hafla ya kukabidhi Pikipiki 125 kwa 'Vijana Sacco's".
Bw. Felix Lwimbo mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi akiwa na Bw. Edmund Ngalawa katika hafla hiyo ya kukabidhi mkopo wa Pikipiki kwa vijana.
"Tunasikiliza maelekezo ya viongozi wetu"
Bw. Felix Lwimbo mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi akimshukuru Mbunge Mgimwa kwa kuwa mdhamini mkuu wa mkopo huo wa Pikipiki kwa Sacco's ya Vijana.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Bw. Nkomola naye akipigilia msumari wa uaminifu juu ya mkopo huo.
Na vichekesho kidogo vilikuwepo, ni vunja mbavu za aina yake zenye ujumbe mkali, zikitolewa na bi. Jesca, akitumia taaluma yake ya ualimu kufikisha ujumbe kwa njia ya Vichekesho.
Jengo la CCM Wilaya ya Mufindi eneo ilipofanyika hafla ya ugawaji wa mikopo ya Pikipiki 125 kwa vijana, ili iweze kuharakisha shughuli za maendeleo na kutoa ajira kwa kundi hilo ambalo ni nguvukazi ya Taifa.
"Waoooo!! Kidumu chama!!!??" Ni kelele za shangwe baada ya vijana hao kufanikisha hafla hiyo kwa kukabidhiwa mikopo ya Bodaboda.
No comments:
Post a Comment