Tuesday, January 7, 2014

KANISA KATHORIKI LAWAONYA VIONGOZI

 Baadhi ya watoto wa marehemu Dr. Willium Mgimwa wakiweka mashada katika kaburi la baba yao mpendwa.
Msinyori wa kanisa Kathoriki Padre Julian Kangalawe akisoma misa takatifu katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa fedha nchini Tanzania, Dr. Willium Mgimwa.
Mafundi wakitandika mbao juu ya kaburi tayari kwa kuweka jeneza lenye mwili wa waziri wa fedha, Dr. Willium Mgimwa.
 Jeneza lenye mwili wa Dr. Willium Mgimwa likipashushwa Kaburini.
 Mke wa marehemu Dr. Mgimwa akiwa ameshikwa na mmoja wa watoto wake wa kike, wakitazama jeneza lenye mwili wa Dr. Mgimwa mara tu baada ya kushushwa kaburini, waliovaa suti kushoto pia ni watoto wa kiume wa marehemu.
 Watawa la kanisa kathoriki wakitazama jeneza (halionekani pichani) likishushwa katika kaburi. (Pembeni hiyo ni meza iliyokuwa imewekewa jeneza).
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na safu ya viongozi wa juu wa kitaifa wakitazama jeneza lenye mwili wa Dr. Mgimwa likishushwa kaburini. (wakwanza kulia ni mama Salma Kikwete, wa pili ni Waziri mkuu Mizengo Pinda akifuatiwa na rais, anayefuata ni Anne Makinda Spika wa bunge, anayefuata ni makamu mwenyekiti wa CCM Mangula, anayefuata ni Willium Lukuvi akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.
 Dada zake marehemu  Dr. Mgimwa wakipeleka taji katika kaburi la kaka yao mpendwa.
 Mama mzazi wa Dr. Mgimwa Bi. Consolata Mgovano akiwa katikati ya watoto zake, kabla ya mazishi ya mpendwa wao Dr. Willium Mgimwa, aliyekuwa waziri wa fedha nchini Tanzania.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akitazama kitabu cha ratiba ya maziko ya Dr. Willium Mgimwa, kulia ni Spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwa na mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista kalalu, katika viwanja vya makaburi ya Ukoo wa akina Mgimwa.

 Jeneza lenye mwili wa Dr. Willium Mgimwa likiwa tayari kwa ajili ya kushushwa katika kaburi.

WANASIASA nchini wametakiwa kuacha tabia ya uongo, kwa kuzungumza mambo yasiyo na uhakika, kwa lengo la kuwadanganya wananchi, kwa madai kuwa tabia hiyo inasababisha taaluma ya Siasa kutoheshimiwa.

Hayo yamezungumzwa na Msinyori wa Kanisa kathoriki, Padre Julian Kangalawe kaimu Askofu mkuu wa jimbo la Iringa, wakati wa mazishi ya aliyekuwa waziri wa fedha nchini Dr. Willium Mgimwa.

Padre Kangalawe amesema wanasiasa wengi wamekuwa waongo na hivyo kuwafanya wananchi kuwa na tegemeo la ahadi zisizotekelezeka, jambo ambalo limeondoa imani kwa jamii juu ya viongozi hao.

Aidha Padre Kangalawe amesema ipo haja kwa viongozi wote kuacha tabia ya kuwabagua watu wenye hali duni ya kipato, na badala yake wawapende wananchi Masikini.

Naye Spika wa bunge Anna Makinda akitoa salamu za bunge amesema Waziri Mgimwa alikuwa ni kiongozi shupavu, mwenye maono ya mbali na mwelevu jambo lililosababisha wizara hiyo kufanya vizuri zaidi.

Hata hivyo Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoa salamu za serikali amesema katika kuyaenzi yote mema ya Waziri huyo serikali itahakikisha inayaendeleza kwa vitendo, yale yote yaliyoanzishwa na Dr. Mgimwa, kwa madai kuwa Waziri huyo alikuwa ni tunu kubwa ya Taifa.
 
Katika mazishi ya Waziri huyo, viongozi mbalimbali wa kitaifa wameweza kuhudhuria huku wakiongozwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwemo pia Waziri mkuu Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, mawaziri wa Wizara mbalimbali, Wabunge, wakuu wa mikoa kutoka mikoa mbalimbali, wakuu wa Wilaya, pamoja na viongozi mbalimbali wa Vyama vya siasa.

"BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE....Amen"
MWISHO

No comments:

Post a Comment