Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Bi. Grace Tendega (kulia) akiwa na mratibu wa CHADEMA kanda ya kusini Bw. Frenk Mwaisumbe- wakijadili jambo.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA walioambatana na mtandao huu wakitoka nje ya nyumba ya mgombea Bi. Grace Tendega, mara baada ya kumalizika kwa mahijiano maalumu baina ya mtandao huu na mgombea ubunge CHADEMA jimbo la Kalenga. Wakitoka nje nyumbani kwa mgombea kijijini Tagamenda- Kalenga.
<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>>>
IMEFAHAMIKA kuwa changamoto kubwa inayowakabiri wananchi wa jimbo la Kalenga Mkoani Iringa ni
upatikanaji mgumu wa pembejeo za kilimo, hali inayosababisha asilimia 89 ya
wananchi wanaojihusisha na kilimo asilimia 70 kuendesha kilimo kisicho na tija.
Hayo
yamezungumzwa na mgombea wa ubunge jimbo la kalenga kupitia tiketi ya Chama cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA Grace Tendega, wakati akifanya mahojiano
maalumu na mmiliki wa mtandao huu nyumbani kwa mgombea huyo kijiji cha Tagamenda.
Tendega
amesema kama wananchi watampa ridhaa na kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo la
Kalenga atahakikisha anaishinikiza serikali iunde chombo kitakachowasaidia
wananchi kupata pembejeo za kilimo hususani Mbolea kwa wakati muafaka.
Aidha
amesema upatikanaji wa pembejeo limekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi wa jimbo
hilo la Kalenga, ana hivyo wananchi na wakulima kwa ujumla kupata shida katika
kuipata mbolea jambo linalodumaza sekta ya kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo
wa Mtanzania.
Amesema
mbolea ambayo inakubalika kwa ardhi ya Kalenga ni DAP huku aina hiyo ya mbolea
ikiwa haipo katika ruzuku ya pembejeo za kilimo na hivyo kujikuta wakipoteza
nguvu zao bila tija kwa kulima kilimo kilichopitwa na wakati ambacho hakitumii
mbolea.
Amesema jambo la kushangaza ambalo hakulifahamu ni uwepo wa vitisho kwa wananchi kuzuiwa kuhudhuria kampeni, ambapo wameelezwa kuwa endapo watamchagua mgombea wa upinzani hawatapata mahitaji kutoka serikalini.
"Kuna jambo kubwa ambalo nilikuwa silifahamu, Sikuwahi kuelewa kuwa wananchi wetu wanawoga, wananchi wamekuwa waoga kwa kuwa wamepewa vitisho vya kuambiwa kuwa endapo mtaipigia kura CHADEMA mtakosa haki zenu, mtakosa huduma muhimu katika jamii kutoka serikalini, lakini ninawaambia wananchi wachague kiongozi wanayemuhitaji katika kuleta maendeleo," alisema Grace.
Hata hivyo
kampeni meneja wa mbunge huyo Alphonce
Mawazo amesema CHADEMA inajivunia kuwa na mgombea makini, mwenye kujenga hoja
na ambaye ni suruhisho la matatizo ya wananchi wa Kalenga, kutokana na kuwa
mzawa wa eneo hilo na hivyo matatizo mengi ya wananchi wa jimbo hilo kuyafahamu.
"Sisi kama CHADEMA tunajivunia sana kuwa na mgombea huyu mwenye upeo mkubwa wa mambo, anafahamu changamoto za wananchi wa jimbo hili la Kalenga, lakini kikubwa kabisa mgombea wetu ni mzawa wa eneo hili, kwa hiyo hata wananchi wakimpa ridhaa ya kuwa mbunge wao anafahamu matatizo yao, tofauti na mgombea wa wenzetu CCM mpaka asimuliwe changamoto za wanaKalenga, yeye kakulia huko nje ya nchi, kujua matatizo ya Kalenga itamchukua muda sana," alisema Mawazo.
Aidha amesema licha ya sifa na vigezo vya mgombea huyo Grace Tendega pia wanaKalenga wanatakiwa wampe kipaumbele mwanamama huyo kutokana na asili yao ya kabila la wahehe kupitia utawala wa Chifu Mkwawa kuwaheshimu wanawake.
Pia amesema ipo haja kwa wananchi kuwaamini wanawake kwa kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuongoza na kupitia hali hiyo, ndiyo maana katika maeneo mengi wanawake wamekuwa watendaji wazuri wa kazi.
Akitolea mfano kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Iringa ambao ni wanawake, Mawazo amesema mkuu wa mkoa wa Iringa ni mwanamke, Katibu tawala ni mwanamke, Mkuu wa Wilaya ya Iringa naye ni mwanamke, mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni mwanamke, mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Mwanamke, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mwanamke pamoja na meneja wa TRA pamoja na viongozi mbalimbali huku katika sekta na idara zao wakifanya vyema kuliko hata wanaume..
MWISHO
No comments:
Post a Comment