Wednesday, August 24, 2011

INUKA NA HUDUMA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

Kituo cha rufaa cha Inuka kinachojihusisha na huduma kwa watoto wenye ulemavu, kimefunguliwa rasmi na waziri wa afya Hajj Mponda ili kuwasaidia wananchi wa nyanda za juu kusini kupata huduma ya matatizo ya watoto wenye ulemavu wa akili na viungo.

Akitolea ufafanuzi wa huduma zinazotolewa, mratibu wa Inuka Bw. Stefano amesema wametoa huduma kwa vijiji 30 katika Wilaya ya Njombe na wanataraji kutoa huduma hiyo kwa mikoa mitano ili kuwafikia walemavu wengi hapa nchini.

Naye katibu mkuu kiongozi Bw. Philimon Luhanjo ameitaka jamii kuacha tabia ya unyanyapaa kwa kundi la walemavu, na kuwapa fulsa za kufanya kazi zinazoendana na ulemavu walionao.

Luhanjo amesema ulemavu si kushindwa kufanya kaz, na kuwa walemavu wanauwezo mkubwa wa kufanya shughuli mbalimbali katika kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchini.

Hata hivyo uongozi wa kituo hicho uliiomba serikali kuwasaidia wataalamu mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa huduma hiyo kwa upana na ufanisi mkubwa.

Waziri wa afya Bw. Mponda aliahidi kusaidia kituo hicho wataalamu pindi tu fulsa inapopatikana.

No comments:

Post a Comment