Katika harakati za kupunguza michango isiyo ya lazima kwa wananchi,mkuu wa wilaya ya Iringa amepiga marufuku michango ya madawati kwa shule za sekondari.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri katika halmashauri ya wilaya ya Iringa,Aseri Msangi ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa amemtaka Afisa Elimu ya sekondari William Mkangwa kusitisha michango kwa wanafunzi wanoanza kidato cha kwanza.
Msangi amewataka wakuu wa shule za sekondari kusitisha michango hiyo mara moja ambayo hutumia kwa kupata fedha za maendeleo kwa shule hizo na kuwataka kubuni miradi mingine ili kuweza kupata fedha hizo.
Hatua ya kupiga marufuku michango ya madawati kwa wanafunzi hao imekuja mara baada ya wajumbe kuhoji sababau za kuchangisha madawati hayo ambayo hutumiwa na wanafunzi hao wawepo shuleni na huyaacha mara wamalizapo shule na kuwa hali hiyo hufanya kuwepo kwa ongezeko la madawati mengi katika shule hizo.
Kwa upande wake Afisa elimu wilaya ya Iringa William Mkangwa amekiri kuwepo kwa wingi wa madawati hayo na kuongeza kuwa kamati ya elimu ilikuwa mbioni kusitisha michango hiyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment