Thursday, May 10, 2012

OFISI YA SHULE YA MGUHU AWALI ILIKUWA HIVI!!



 

WANAFUNZI  wa shule ya Msingi MGUHU, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wakipita nje ya ofisi ya walimu, iliyojengwa kwa nyasi. 

Shule ya Msingi iliyopo katika Wilaya ya Iringa, katika kijiji cha Nyabula, ambayo mnamo mwaka 2000 hadi mwaka 2011 walikuwa wanasomea katika uzio wa Nyasi, huku walimu wao wakikaa katika banda hilo la nyasi.

Moja ya changamoto iliyokuwa ikiikabili shule hii ni pamoja na ukosefu wa vyoo vya walimu, na hivyo walimu kukosa huduma hiyo ya muhimu.

Lakini kutokana na jitihada za wananchi na uongozi wa Halmashauri hiyo zimefanikisha kujenga vyumba vya madarasa, viwili, vyoo vya walimu pamoja na ofisi za walimu, jambo linalowafanya wanafunzi hao kuepukana na adha waliyokuwa wakiipata awali ya kusomea katika uzio wa nyasi.


No comments:

Post a Comment