.
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,kushoto ni mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Evarista Kalalu, akiwa mgeni rasmi wa kikao cha baraza la madiwani
Madiwani wakisikiliza kikao namna kinavyoendelea.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufundi katika mkoa wa Iringa wamevitaka vyombo vya sheria kama taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa na jeshi la polisi, kuwachukulia hatua stahiki mawakala wote waliojihusisha na utapeli na ufujaji wa fedha za serikali kwa kushindwa kufikisha pembejeo za kilimo kwa wakulima wilayani humo.
Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, na kuhudhuliwa na madiwani wa kata mbalimbali pamoja na wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo.
Akilalamikia mawakala hao mmoja wa madiwani hao Mh. Evaristo Lukunga wa Kata ya Ikweha, amesema mawakala hao wamediliki kutumia hata majina ya watu waliofariki siku nyingi kuorodheshwa katika idadi ya waliochukua pembejeo za kilimo.
No comments:
Post a Comment