1- Oliver Motto, mmiliki wa Blog (Star Tv Rfa $ gazeti Mtanzania)
2- Daud Mwangosi- Chanel Ten, na Magic Fm
3- Frenk Leonard- Habari leo na Daily news
4-Fransis Godwin- Tanzania daima na magazeti mengine
5- Sima Bingileki- IMTV
Tukiwa na marehemu Mwangosi, nje ya Meli kabla ya kuanza safari ya kwenda Pemba.kulia ni Oliver Motto, (katikati) Marehemu Mwangosi) na kushoto ni Sima Bingileki- tulitakiwa kuva mavazi hayo kulingana na masharti ya huko tuendako, wengine shungi zilitushinda, lkini ilitulazimu kufanya hivyo.
Mwangosi (aliyesimama) na Oliver Motto,(Mwenye ushungi) wakiwa ndani ya Meli wakipunga upepo nje ya Meli huku wakiendelea na safari, pembeni ni wasafiri wa kigeni(Mzungu).
Ndani ya chopo kulikuwa na watu mbalimbali, hapo Mwangosi akiwa na Dude, msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu.
Marehemu Mwngosi (anayepiga picha) akiwa na Oliver Motto( aliyeshika Mic) wakifanya mahojiano na mmoja wa wadau wa habari.
Frances Godwin mmoja wa wasafiri wa chombo hicho cha majini kuelekea Pemba, ni mmoja wa watu wa jirani na marehemu Mwangosi
Oliver Motto,nikiwa kando ya bahari ya Hindi, Pemba jirani na eneo la Shumba, Daud Mwngosi nilifanya nae kazi mara kwa mara,na maeneo mengi sana, alikuwa nio mtu wangu wa karibu sana kikazi, ushauri wa kikazi na kimaisha, kwani Mwangosi alikuwa kama Mwalimu, kuna wakati alitufundisha, kutuonya na kutusihi.
Hapo tumerejea safarini, ni bandarini jijini Dar es salaam, ni majira ya saa mbili usiku. Daud Mwangosi wa kwanza kushoto, anayefuata ni Fransis Godwin, Sima Bingileki na Oliver Motto.
Tukiwa Shumba Pemba tulikutana na wavuvi, na huyu ni mmoja wa samaki anayepatikana katika Bhari ya Hindi.
No comments:
Post a Comment