Wednesday, September 12, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA DAUD MWANGOSI ATINGA MAHAKAMANI KWA MBWEMBWE




Picha-: Marehemu Daud Mwangosi enzi za uhai wake.

MTUHUMIWA wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Luninga ya Chanel Ten Bw. Daud Mwangosi, amefahamika leo mahakamani kuwa ni askari Pacificus Cleophace Simon (23) ameingia leo kwa bwebwe katika viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Iringa, baada ya gari la kifahari aina ya Land Cruser (Shangingi) nyeupe yenye namba za usajili T320ARC likisindikizwa na Land Cruser pic up, huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi.

Simon aliyetambuliwa kwa namba G2573 mkazi FFU Iringa   amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu na waliovaria sare wakiwa na siraha zaidi ya 10, ambao walikuwa wakimzuia hadi wanahbari kushindwa kupata picha y mtuhumiwa huyo.

Akisomewa shtaka mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Mheshimiwa Dyness Lyimo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkuu,mwanasheria Michael Luwena alisema inadaiwa kuwa Pacificus Cleophace Simon alitenda kosa hilo Septemba, 2 mwaka huu eneo la Nyololo wilayani Mufindi.
Kesi hiyo ni ya mauaji  ya kukusudia imefunguliwa chini ya kifungu 196, kanuni za adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002, Kwa mujibu wa kesi za mada mtuhumiwa hakurusiwa kujibu chochote.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Dyness Lyimo alisema mahakama ya mkoa haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji hivyo ni kusoma tu.Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 26, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment