Wednesday, September 25, 2013

WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WAJIUNGA NA VYUO


Wakuu wa vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (Veta) wakiwa katika ukumbi wa chuo cha Donbosco mjini Iringa, wakipatiwa elimu ya ujasiriamali.
 Bw. Yonah Sanga mkuu wa chuo cha Coritech cha mjini Iringa akiwa katika mafunzo ya ujasiriamali, yaliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya ufundi stadi cha Donbosco mjini Iringa. 
             Washiriki wakisikiliza jambo kwa umakini mkubwa. 
 Padre Abery Njeru mkuu wa chuo cha Ufundi Donbosco cha majini Iringa akiwa na katika ukumbi wa mafunzo ya ujasiriamali, yaliyofanyika katika chuo chake, kwa kuwakutanisha wakuu wa vyuo vya ufundi kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini.
Bw. Eugen R. Mgaya mkuu wa chuo cha ufundi cha  Education and Entrepreneurship Ltd  (E&E) cha mkoani Njombe, akiwa na mshiriki mwingine katika mafunzo ya ujasiliamali ya wakuu wa vyuo vya ufundi wa nyanda za kusini.



WAKATI jamii ikipigwa na butwaa juu ya uwepo wa wanafunzi wa elimu ya sekondari kutokujua kusoma na kuandika, baadhi ya wanafunzi wa vyuo nao wanakumbwa na jinamizi hilo la kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi Veta huku wakiwa hawafahamu kuandika wla kusoma.


Wakizungumzia tatizo hilo, wakuu wa vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi VETA, wakati wa mkutano wa walimu na wakuu wa vyuo vya ufundi kanda ya kusini, mkutano uliofanyika katika chuo cha mafunzo ya ufundi stadi Donbosco mjini Iringa, walimu hao wamesema moja ya changamoto inayowakabili kwa sasa ni tatizo la wanavyuo kutojua kusoma na kuandika.

Evalisto Mtitu mkuu wa chuo cha ufundi Mlando kilichopo mjini Makambako na Yona Sanga mkuu wa chuo cha Coritech cha mjini Iringa wamesema vyuo vyao vinakabiliwa pia na tatizo hilo la uwepo wa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.

"Ni kwamba wanafunzi hawa tupo nao lakini huwa tunawagroup katika makundi mawili, kundi la wasiojua kusoma na kuandika ni Slow Lenners na wanaojua kusoma na kuandika wanakaa katika kundi la Faster Lenners, lakini hawa wasiojua kusoma na kuandika wanafaa zaidi katika ufundi stadi, kwani nguvu zao za akili wanakuwa wamezielekeza sana katika vitendo kuliko hawa wanaojua kusoma na kuandika, wanajuhudi kubwa katika kukarili mambo wanayoelezwa na walimu," alisema Sanga.

Naye Padre Abery Njeru, mkuu wa chuo cha ufundi na mafunzo stadi Donbosco cha mjini Iringa, amesema uelewa wa wanavyuo wasiojua kusoma na kuandika ni mkubwa katika mafunzo ya vitendo kuliko nadharia.
 
Padre Njeru amesema chuo hicho ni msaada kwa kundi la watu wa aina hiyo, ili kuwapa fulsa ya kupata ujuzi wa kuendesha maisha yao pasipo kuwatenga, kwani wamekuwa wakifanya vizuri katika kitengo cha mafunzo kwa vitendo ukilinganisha na wale wanaojua kusoma na kuandika.

"Chuo hiki cha Donbosco kilianzishwa hasa kuwasaidia hao, kwani hawapewi kipaumbele zaidi katika jamii, sisi hapa hatuwabagui tunawachukua wote, wale wa darasa la saba na wakidato cha nne ili kutowafanya wasijisikie tofauti zaidi na wa kidato cha nne, na pia kimatendo wa darasa la saba wako juu zaidi kuliko wa kidato cha nne, hata katika mitihani tunawachanganya ili pale wanapokosea tuwasahihishe, na mafunzo tunawapa yale yale, na jamii inatakiwa kuwapatia moyo zaidi kwa kuwafuatilia siku hadi siku ingawa ni vigumu sana kujenga jengo pasipokuwa na msingi imara, hii ni kwamba ni vigumu sana kuwafundisha lakini wengine wanaakili ya kuzaliwa nao, wanakuwa vizuri sana kwenye vitendo," alisema Njeru.
 Hata hivyo elimu hiyo ya ufundi ni msaada mkubwa hata kwa kundi hilo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika, kwani elimu hiyo ya vitendo itawaongezea ujuzi na ufanisi katika kuanzisha ajira binafsi baada ya kujifunza masuala mbalimbali ya ufundi, ubunifu na ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali.
MWISHO


No comments:

Post a Comment