Mkuu wa chuo kikuu cha Iringa Profesa Nicolas Bangu akipokea tuzo ya heshima ya haki za binadamu, kutoka kwa muhadhiri wa kitivo cha sheria Jane Massey, tuzo ambayo imekiletea heshima chuo na Taifa kwa ujumla.
Kulia ni muhadhili wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha sheria Jane Massey akiwa na wanafunzi wanne walioshiriki mashindano ya kuipata Tuzo hiyo ya heshima ya kimataifa ya haki za binadamu, iliyotolewa na chama cha msalaba mwekundu.
Tuzo ya heshima ya haki za binadamu ya Kimataifa ya "Henry Dunant" iliyozishirikisha nchi mbalimbali za Afrika ikiwa pamoja na vyuo mbalimbali nchini, ambapo chuo kikuu cha Iringa kimeweza kuibuka kinara wa mashindano hayo.
Kushoto ni mwanafunzi Joanna Mcintyre mshiriki wa tuzo hiyo ya heshima akiwa na wanafunzi wenzie na wahadhiri Kulia ni Jane Massey muhadhiri mkuu wa kitivo cha sheria, wa katikati ni Janeth Nagai, Anneny Nahum ambaye pia ni mwanafunzi mshiriki wa kuipata tuzo hiyo pamoja na Henry Mwinuka muhadhiri wa kitivo cha sheria katika chuo hicho cha Iringa.
CHUO kikuu cha Iringa ambacho awali kilichofahamika kama Tumaini, kimetunukiwa tuzo ya heshima ya Taifa na Afrika,ya Henry Dunant ambaye alikuwa mwanzilishi wa kutetea haki za binadamu wawapo vitani , ili kuwaepusha waathirika wa majanga ya vita na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ukiwemo ubakaji.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa na chama cha msalaba mwekundu, ikiwa sasa ni mara ya 16 tangu ianzishwe, huku ikivishirikisha vyuo vikuu mbalimbali nchini, ambapo chuo cha Iringa kimefanikiwa kuichukua tuzo hiyo.
Anneny Nahum, Janeth Nagai na Joanna Mcintyre washiriki wa mashindano hayo wamesema hatua hiyo niya kujivunia, ikiwa pamoja na wahusika wa masuala ya amani kutovunja sheria za haki za binadamu za kimataifa pindi wawapo vitani.
Jane Massey mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria amesema tuzo hiyo ya heshima ya Henry Dunant ambaye ni muanzirishi na muhusika mkuu wa haki za binadamu wakati wa vita na kuwa tuzo hiyo ni alama kuu ya kuonyesha Taifa la Tanzania inaufahamu mkubwa wa masuala yahusuyo haki za binadamu za kimataifa.
Aidha Massey amesema vyuo vilivyoshiriki katika mashindano hayo ni chuo kikuu cha Ruaha Iringa(RUCO, chuo kikuu cha Dar es salaam, Chuo cha Sauti Mzumbe Morogoro na chuo kikuu cha Iringa, huku nchi za afrika zilizoshiriki ikiwa pamoja na Zimbabwe, Afrika kusini, Ruanda, Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania ambayo ndiyo imeibuka mshindi..
Naye Profesa Nicolas Bangu mkuu wa chuo hicho cha Iringa amesema tuzo hiyo ni kielelezo kimataifa kuwa Tanzania ni kitovu cha amani kutokana na ufahamu mkubwa wa haki hizo za binadamu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment