Mtaa wa Uhindini moja ya mitaa ambayo siku za kawaida huwa na msongamano wa watu mjini Iringa.
Mtaa wa Mantigo au Miyomboni kati ya mitaa ambayo nayo siku za kawaida huwa na msongamano mkubwa wa watu mjini Iringa.
Hapa ni katikati ya mji wa Iringa- panaitwa mtaa wa Kongo, eneo la stendi ya daladala, nako hali ndiyo kama hii unavyoiona- maeneo haya huwa na mrundikano mkubwa wa watu mjini Iringa.
hapa ni eneo la barabara Pacha za Mwembetowa Stendi kuu, nako hali halisi kama inavyoonekana maduka nayo yamefungwa.
WAFANYABIASHARA
mkoani Iringa wamegoma kufungua maduka, huku
biashara mbalimbali za kiuchumi zikisitishwa, kwa kile wanachodai kuwa
kufanyiwa usumbufu uliokithiri na baadhi ya watumishi wa wanaitaka
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), zikiwemo mzigo wa kodi unaowaelemea.
Mgomo huo ambao umeanza mapema alfajiri ya siku ya leo, huku baadhi ya
wanaofungua huduma za kibinadamu nao wakishinikizwa kutotoa huduma hizo, unachangiwa pia na mashine za Kielectreonic za EFD za kutolea Stakabadhi pindi tu mteja anaponunua bidhaa .
Wakizungumzia
mgomo huo baadhi ya wafanyabiashara hao
wamesema mgomo huo umefikiwa baada ya kutosikilizwa kilio chao, huku
kukiwa na mkanganyiko kati ya wafanyabiashara wa kariakoo jijini dar es
salaam kusitishiwa utaratiubu huo mpya wa TRA wakati wao wa mikoani
wanaonunua bidhaa zao zote kariakoo wakitakiwa kuwa na kumbukumbu za
manunuzi.
"Hebu
ona ndugu mwandishi, kule Kariakoo wanunuzi wanaotuuzia mali hizi zote
kutokja mikoa wamepewa muda wa kuendelea na utaratibu wao wa zamani wa
kutotumia mashine za EFD, lakini sasa sisi tunapokuja huku mikoani hawa
TRA wanasema hawaelewi hilo tunatakiwa kuambatanisha kwenye malipo
manunuzi yetu, sasa sisi tunatoa wapi wakati wafanyabiashara wakubwa dar
hawatupi risiti??," Alihoji Tito Kalole.
James Mdegipala mmoja wa wafanyabiashara hao amesema ipo haja kwa TRA pia kuwasikiliza malalamiko yao juu ya
gharama kubwa za ununuzi wa mashine hizo.
Makey Masharo amesema wataendesha mgomo huo mpaka malalamiko
yao yatakaposikilizwa kwani baadhi ya wafanyabiashaea wameingiwa na hofu juu ya tishio la upandishaji wa kodi kwa asilimia 18.
Jackson
Kalole naye amesema serikali inapaswa kushirikiana na wadau wake pindi
inapotaka kufanya mabadiliko, hasa yanayohusu uchumi wa nchi ili
kuondokana na changamoto hizo, kwani licha ya kuwepo kwa kodi zaidi ya 9
kwa mfanyabiashara mdogo wa duka, kumekuwa na tatizo la elimu juu ya
ongezeko la kodi hizo.
Aidha
wafanyabiashara hao wamesema hawapo tayari kufungua maduka yao, hadi
pale serikali itakapoona umuhimu wa kukaa meza moja na wao ili kumaliza
changamoto hizo.
Naye Lukas Mwakabungu mwenyekiti wa chama cha
wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima TCCIA amesema chemba hiyo haihusiki
na mgomo huo na kuwa atakaa na wafanyabiashara hao ili kutambua sababu za wao
kugoma.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma
amewataka wafanyabiashara hao kufungua maduka yao, kwa madai kuwa huo ni mkumbo
wa baadhi ya vijana wanaochochea wenzao kutofungua maduka.
Hata
hivyo wafanyabiashara hao wametawanywa na jeshi la polisi mara tu
walipojaribu kutaka kukusanyana ili kujadili hatma ya tatizo hilo,
ambapo wameitaka serikali kuona hasara inayoingia kwa kushindwa
kukusanya kodi katika siku watakazokuwa wamesusia kufungua maduka na
kutoa huduma kwa jamii.
MWISHO.
Jumamosi, 4 Januari 2014
"FAWE na TUSEME" MARUFUKU WATOTO KUTUMIKISHWA KATIKA AJIRA
Baadhi ya watoto washiriki wa kongamano
la kambi lililoandaliwa na shirika la FAWE kwa kushirikiana na UNICEF
chini ya mradi wa TUSEME, kambi iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ.
Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Bi. Neema Kitundu- mratibu wa FAWE Taifa
akisikiliza maoni ya watoto katika kambi iliyowakutanisha watoto wa
shule za msingi kutoka Wilaya sita, - Wilaya ya Makete, Mbeya Vijijini,
Mtwara, Temeke, Mufindi pamoja na Iringa vijijini.
Bi.
Sophia Komba mmoja wa viongozi wa mradi wa FAWE akizungumza na jopo la
watoto wa shule za msingi kutoka katika Wilaya sita nchini, katika kambi
iliyofanyika katika shule ya sekondari JJ. Mungai Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Baadhi
ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la
FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, wakionyesha
ubunifu wao wa kuchora michoro inayoendana na mafunzo ya kupinga ukatili
na unyanyasaji wa watoto, ambao unachangia baadhi yao kuikosa elimu.
Baadhi
ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la
FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, kambi
iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ. Mungai katika Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Baadhi
ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la
FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, kambi
iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ. Mungai katika Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Baadhi ya walimu ambao waliambatana na wanafunzi wao katika kambi hiyo
wakisikiliza maoni ya wanafunzi hao juu ya ukatili wanaofanyiwa.
Watoto kutoka Wilaya ya Temeke wakitoa ushuhuda kupitia maigizo kama ni sehemu ya ushiriki wao katika kambi hiyo.
Watoto
washiriki wa kambi la wanafunzi kutoka Wilaya sita nchini wakitoa
ushuhuda juu ya vitendo vya ukatili vilivyopo katika jamii wanamoishi.
SHIRIKA la FAWE chini
ya mradi wake wa TUSEME nchini Tanzania limepiga
marufuku mtindo wa baadhi ya wazazi na walezi kuwatumikisha watoto wenye umri
wa kwenda shule, katika shughuli mbalimbali ambazo ni kikwazo katika elimu.
Hayo yamezungumzwa na
mratibu wa FAWE nchini Bi. Neema Kitundu katika kongamano la watoto wa
shule za msingi kutoka Wilaya tisa nchini, ambapo amesema tatizo la watoto
kutumikishwa bado lipo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, pamoja na Wilaya
ya Mbarali mkoani Mbeya.
Bi. Kitundu amesema tatizo
hilo halina tofauti na ukatili wa kijinsia, na kuwa hali hiyo imeshamiri sana katika
Wilayani Mufindi ambapo watoto hutumikishwa kama vibarua katika mashamba ya
Chai, huku wengine wakitumiwa katika ajira za kazi za nyumbani.
Aidha Bi. Kitundu amesema
katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya nao wanaukatili kwa watoto hao wadogo, na
kuwa wao huwatumia watoto katika mashamba ya Mpunga, jambo linalowafanya wakose
kwenda shule.
“Tumeona bado kuna changamoto
kubwa kwa watoto hawa, na katika wilaya
tunazozifanyia kazi tumetambua Wilaya ya Mufindi inawatumikisha watoto katika
mashamba ya Chai, huku Wilaya ya Mbarali watoto wengi wanafanyishwa kazi katika
mashamba ya Mpunga, jambo hili ndugu zangu linakwamisha sana sekta ya elimu, na
halina tofauti na ukatili wa kijinsia, kwani watoto hawa wanaikosa fulsa muhimu
ya elimu,” Alisema Kitundu.
Amesema baadhi ya
watoto wamekuwa wakitoroka shule na hata kutokwenda kabisa na kukimbilia katika
ajira hizo na hivyo kupoteza muda wa masomo, jambo ambalo linaashiria
kukosekana kwa elimu kwa watoto hao na hivyo Taifa kuwa na watu wasio na elimu.
“Katika Wilaya ambazo
tumezifikia tatizo la ajira za utotoni tumetambua bado zipo kwa Wilaya ya
Mufindi na Mbarali, na wengi wetu hasa tunaotoka Dar es Salaam tumekuwa na
dhana ya kuwa wasichana wa kazi za ndani wazuri wanatoka Mufindi Iringa, na
kule Mbarali wao wanajihusisha sana na kilimo cha Mpunga, na wakati wa kilimo
watoto wengi wanashinda mashambani, na hata wazazi wapo radhi kuomba ruhusa
shuleni kwa kisingizio kuwa mtoto swake anaumwa kumbe anamfanyisha kazi za
shambani, si wavulana si wasichana” Alisema
Amesema FAWE kwa
kushirikiana na UNICEF walifanya kazi kwa wilaya kumi, na sasa wameanza na
Wilaya sita ambazo ni Wilaya ya Makete, Mufindi, Njombe, Mbeya vijijini, Iringa
Vijijini na Wilaya ya Mbarali.
Amesema mradi FAWE kwa
kushirikiana na UNICEF umeweza kuleta mafanikio makubwa, kwa kupunguza tatizo
la wanafunzi wa kike kuacha masomo kwa kupata mimba, ambapo mwaka 20006 kabla mradi haujaanza kufanyakazi mimba
zilikuwa zaidi ya 400 kila mwaka kwa shule za msingi pekee, na shule zilizokuwa
ndani ya mradi wa FAWE mimba zilikuwa 166 kwa mwaka, na mafanikio yamepunguza
tatizo hilo la mimba hadi ambapo mwaka 2013 mimba zimebaki tatu pekee.
Naye mwasisi wa FAWE
nchini Profesa Penina Mrama amesema FAWE kwa kushirikiana na TUSEME inamsaidia
mtoto kupata elimu ya utambuzi wa haki zake za msingi na kuondoa ubaguzi baina
ya watoto wa kike nawa kiume.
Profesa Penina amesema
kupitia mradi wa FAWE na TUSEME wameweza
kuwaokoa watoto wengi ambao walikuwa tayari wameikosa elimu, na sasa wamejikita
zaidi kulielimusha kundi hilo kutambua haki zao ili waweze kuzitetea.
Na
kuwa shirika limekuwa likitoa afua za kusaidia sekta ya elimu kwa
kujenga miundombinu wezeshi kama Maktaba, Maabara, Mabweni y Chakula,
utoaji wa Vitabu nk. yote hayo yakiwa yamelenga kuyafanya mazingira ya
elimu kuwa rafiki kwa wanafunzi ili kuvutia na kuipata elimu pasipo na
vikwazo vovyote.
Aidha Profesa Penina
amesema pia mradi unapingana na vitendo vya ukatili vinavyochangia mtoto
kushindwa kupata elimu, zikiwemo ajira pingamizi kwa sekta ya elimu.
Hata hivyo shirika la kazi
duniani (ILO) katika ripoti yake iliyotolewa mjini Geneva kuna zaidi ya watoto milioni 10.5
duniani wanatumikishwa kazi za nyumbani katika mazingira
magumu.
Katika ripoti hiyo Shirika la Kazi Duniani ,limeeleza kwamba watoto hao wanafanya kazi za usafi, wanapika,wanatunza bustani na pia wanafanya kazi ya uyaya, hiyo ikiwa haina tofauti kabisa na ripoti ya FAWE katika Wilaya zake inazozifanyia kazi, ambako changamtoto hizo za kazi kwa watoto nazo zimejitokeza kwa kiwango kikubwa.
ILO ilienda mbali zaidi na kusema katika ripoti yake kuwa watoto milioni sita na nusu wanaofanyishwa kazi za majumbani wana umri kati ya miaka 5 na 14 na zaidi ya asilimia 71 ni wasichana.
Katika ripoti hiyo Shirika la Kazi Duniani ,limeeleza kwamba watoto hao wanafanya kazi za usafi, wanapika,wanatunza bustani na pia wanafanya kazi ya uyaya, hiyo ikiwa haina tofauti kabisa na ripoti ya FAWE katika Wilaya zake inazozifanyia kazi, ambako changamtoto hizo za kazi kwa watoto nazo zimejitokeza kwa kiwango kikubwa.
ILO ilienda mbali zaidi na kusema katika ripoti yake kuwa watoto milioni sita na nusu wanaofanyishwa kazi za majumbani wana umri kati ya miaka 5 na 14 na zaidi ya asilimia 71 ni wasichana.
Pia ILO ilibainisha kuwa watoto wengi wanaoajiriwa majumbani mara nyingi hawalipwi ujira
stahiki na waajiriwa wao, huku baadhi ya waajiri wakidiliki hata kuwabagua ,
jambo linalojenga dhana potofu katika vichwa vya Taifa hilo la kesho.
Na hali hiyo ya ajira kwa kundi la watoto isipopigiwa kelele inaweza kuongezeka zaidi kila mwaka kutokana na mahitaji ya watumishi wa nyumbani, kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanajishughulisha na kazi mbalimbali na hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa wafanyakazi wa kazi za nyumbani.
Huenda hali hiyo ya
ajira kwa kundi la watoto wadogo likaongezeka zaidi na zaidi kutokana na wanawake
wengi kupata kazi nje ya nyumba hali
inayotofautiana na siku za awali ambapo mwanamke alionekana kuwa ndiye muhusika
mkuu wa kazi za nyumbani za kuihudumia familia.
MWISHO
Jumatatu, 30 Desemba 2013
BARABARA YA HIFADHI YA RUAHA YAKWAMISHA UTALII
Wadau wa sekta ya Utalii wakisikiliza
jambo katika moja ya vikao vya kujadili mikakati ya namna ya kuendeleza
sekta hiyo ambayo ni kiini cha Pato la Taifa.
Mmmoja
wa viongozi wa mradi wa SHICs unaojihusisha na kuendeleza utalii wa
mila na tamaduni mikoa ya Kusini (Iringa) akifafanua jambokatika ukumbi
wa chuo kikuu cha Iringa, ambapo wadau wa sekta hiyo ya Utalii
walikutana.
Yan
Kuva meneja wa mradi wa SHICs unaojihusisha na kuendeleza utalii wa
mila na tamaduni mikoa ya Kusini (Iringa) akifafanua jambo katika chuo
kikuu cha Iringa, ambapo chuo hicho kimepewa dhamana hiyo.
MIUNDOMBINU mibovu, ajira za kindugu zisizozingatia utaalamu
na kauli zisizofaa, ni moja ya vikwazo vinavyoikwamisha sekta ya utalii mkoani
Iringa, licha ya mkoa huo kupewa heshima ya kuwa kitovu cha Utalii nyanda za
juu kusini.
Hayo yamezungumzwa na wadau wa sekta ya Utalii mkoani Iringa,
katika kikao chenye lengo la kuendeleza Utalii wa mila na tamaduni za jadi, lengo
likiwa ni kuwavutia watalii walio wengi
kufika mkoani humo kujifunza maisha ya awali ya makabila ya mkoa wa Iringa, na
hatimaye fedha za mapato ya watalii kusaidia kukuza uchumi na pato la Taifa.
Steven Mhapa ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya
Iringa na mdau wa utalii amesema ubovu wa barabara inayoelekea katika Hifadhi
ya Taifa ya Ruaha ni changamoto kubwa katika kuyafikia malengo ya kuinua sekta
ya utalii mkoni Iringa.
“Tunafahamu barabara barabara ni kiungo muhimu sana katika
kuwafikisha watalii katika hifadhi, sasa barabara yetu ya Ruaha si rafiki
kabisa kwa vivutio vya utalii, na kutokana na hali hiyo baadhi ya watalii wenye
uwezo huamua kukodi usafiri swa anga yaani Ndege, huku wenye kipato cha kawaida
wakitumia usafiri wa barabara, ambapo hao wamekuwa wakilalamikia sana barabara
hiyo na hivyo pindi wanapomaliza utalii wao huwa hawarudi tena, ipo haja ndugu
zangu kujipanga vyema hasa katika miundombinu ya barabara,” Alisema.
Afisa utamaduni Wilaya ya Iringa Bi. Joyce Nachilima amesema
hata masuala ya utandawazi nayo yanabainishwa kuwa yanachangia baadhi ya vijana
kutohitaji tena mambo ya mila na tamaduni za jadi, kuanzia mavazi na hata
vyakula, wakihitajika vile tu vinavyokwenda na wakati.
“Vijana wetu wengi siku hizi wanafikilia tu kutunga nyimbo za
Bongo fleva ambazo ndiyo zinaitwa za
kizazi kipya, na unapowaambia wabuni nyimbo za jadi kama Mangala na Kiduo nyimbo
za asili kwa makabila yao wao wanaona kama ni masauala yaliyopitwa na wakati,
sasa jambo hilo linakuwa ni gumu sana kufanikiwa maramoja katika sekta ya
Utalii wa tamaduni,” Alisema.
Naye Hawa Mwechaga afisa utalii Wilaya ya Iringa amesema wananchi
mkoani Iringa wanapaswa kuanza wenyewe kuvitangaza vivutio vya mila na tamaduni
za makabila yao, ikiwa pamoja na kuendelea kuvaa mavazi aina ya “Migolole”
ambayo yalivaliwa na machifu wa kabila la Wahehe, na kuacha tabia ya kuiga
mavazi ya makabila mengine kama ya Wamasai.
Hata hivyo Jimson Sanga ambaye ni katibu wa mradi wa
kuendeleza Utalii wa mila na tamaduni mkoa wa Iringa, amesema wananchi mkoani
humo wana fulsa nyingi katika kuboresha utalii, hasa kubwa ikiwa ni kipaumbele cha
mkoa wa Iringa kupewa heshima ya kuwa ni kitovu cha Utalii nyanda za juu
kusini.
MWISHO
Jumatano, 18 Desemba 2013
KATIBU TARAFA AHIMIZA UJENZI WA VYOO BORA
Waziri
Lukuvi akijaribu moja ya Pikipiki huku katibu tarafa Mwaulesi
akiangalia kitendea kazi hicho, ambapo Waziri huyo alikabidhi Pikipiki
nne ambazo kati yake zilipelekwa tarafa ya Isimani na Idodi.
KATIBU tarafa wa tarafa
ya Pawaga Mkoani Iringa Bw. Nasson Mwaulesi amewataka wananchi kujenga vyoo bora na vya mfano
ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu.
Akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Kimande, katibu tarafa huyo amesema hakuna njia mbadala ya
kukwepa magonjwa ya matumbo pasipo kuboresha mazingira ukiwemo ujenzi wa vyoo hivyo bora.
Aidha Mwaulesi amesema
ili kufanikisha mpango huo na kuondokana na vyoo duni atahakikisha ofisi ya afya
wilaya ya Iringa inapeleka mchoro wa choo bora kinachotumia ujenzi wa gharama
nafuu, ukiwa ni msisitizo wa kuachana na matumizi hayo ya vyoo duni .
"Kuna
vyoo vya ajabu sana hapa, vilivyo vingi hata mlango havina, wengine
wameweka magunia katika vyoo vyao, na baadhi ya nyumba hazina vyoo
kabisa, uongo??...Sasa jamani achaneni na tabia hiyo, kwani uzuri wa
nyumba ni choo," Alisema.
Pia
aliwataka wananchi na ofisi za vijiji vyote 12 vya tarafa hiyo ya
Pawaga kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo ifikapo April mwaka
2014, ambapo alimuagiza mkuu wa Polisi tarafa ya Pawaga kuwachukulia
hatua za kisheria wananchi wote watakaokaidi agizo hilo.
Hata hivyo mbunge
wa jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi
ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Mh. Wiliam Lukuvi akikabidhi
gari la wagonjwa lenye thamani ya
zaidi ya Tsh milioni 180 katika kituo cha afya Kimande Pawaga
amewataka wananchi hao kujiunga na mpango wa huduma ya afya jamii (CHF) ili
kuepukana na gharama kubwa za matibabu.
Waziri
Lukuvi pia alikabidhi Pikipiki nne zenye thamani ya zaidi ya shilingi
Milioni saba, ambapo Pikipiki mbili zilikuwa ni ahadi ya mh. rais Jakaya
Kikwete na mbili zilinunuliwa na Waziri Lukuvi, kwa ajili ya
ufuatiliaji wa miundombinu ya mradi wa maji bomba.
Katika
kuhakikisha wananchi hao hawana vyoo bora Waziri Lukuvi alishindwa kumpata
mwananchi hata mmoja mwenye choo bora cha mfano katika kijiji hicho, hatua
iliyoonyesha baadhi ya wananchi hao kutolitilia mkazo suala hilo la ujenzi wa
vyoo bora.
MWISHO
No comments:
Post a Comment