Saturday, March 26, 2011

KAPUNGA RICE WAOMBA KUWEKEWA MIPAKA NA SERIKALI


Jengo hili ni ghara la kampuni ya kapunga Rice lililopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kampuni ambayo inayojihusisha na kilimo cha Mpunga na uuzaji wa mchele bora.


Kampuni ya Kapunga iliyopo katika Wilaya ya Mbarali koani Mbeya imeiomba serikali kuweka mipaka kati ya shamba la mwekezaji na eneo la wananchi.

Akizungumzia mpango huo ofisa utawala Peter Chacha amesema kutofahamu ukomo wa maeneo yao kati ya shamba la mwekezaji na wananchi kunachangia kudumaa kwa maendeleo ya kijiji na kampuni.

Chacha amesema hali hiyo inachangia malumbano kati ya pande hizo mbili kwa kukosa ufahamu wa ukomo wa haki ya ardhi zao na kila mmoja akafanya shughuli za maendeleo kwa kutambua mipaka yake.

No comments:

Post a Comment