Wananchi wameitaka serikali kutoa taarifa na mapema na elimu juu ya uvunjaji wa majengo yaliyowekwa alama (X) inayoashiria jengo kubomolewa kwa kuwepo katika hifadhi ya barabara.
Wito huo umetolewa na wananchi wa Wilaya ya Makete wakati wa mdahalo unaohusu utawala bora ulioandaliwa na asas ya Iringa Civil Society Organizatios (ICISO) uliofanyika Wilayani Makete.
“Tunamshanga mkurugenzi anapotuambia tunatakiwa kuondoka kwenye nyumba zetu eti kwa sababu zimewekwa alama ya “X” wakati hajatujaonyesha sehemu ya kwenda,hajatupatia elimu juu ya utaratibu huo, anataka tukaishi wapi?”, Walisema.
Wananchi hao walisema serikali huamua kubomoa majengo hayo bila kutoa elimu ya umuhimu wa kufanya shughuli hiyo na kujenga chuki baina yake na wananchi.
Mchungaji Akimu Mwandilla kutoka katika kanisa la kiluther Wilayani Makete amesema kupitia mpango huo Halmashauri ya Wilaya ya Makete hutumia nguvu katika kutekereza majukumu yake bila kutoa elimu kwa jamii juu ya zoezi la boamoaboamoa na wananchi wakinyimwa fulsa hiyo ya kuelimishwa.
Wamesema Halmashauri imekuwa ikiongeza vipimo vya X katika upanuzi huo kwa madai ya upanuzi wa barabara pasipo kuwaeleza wananchi malengo na manufaa ya bomoabomoa hiyo na kusababisha wananchi kuwa na chuki na serikali yao.
Wamehoji kuwa wananchi wanaokumbwa na tatizo hilo wamewekewa mbadala gani juu ya makazi hayo yanabomolewa kwani mpango huo utawaathiri na kuwarudisha nyumba kimaendeleo kwa kuanza kunua viwanja na kujenga nyumba zao upya.
Wameitaka Halmashauri kutoa taarifa za maendeleo yao kupitia mikutano ya hadhara ili kila mmoja awaze kusikia tofauti na utaratibu wa sasa, na kuwa baadhi ya nyumba zimeathiliwa na zoezi hilo na kulazimika kubomolewa jengo lote .
Diwani wa Kata ya Kipagalo ambaye awali alikuwa katibu tarafa wa kata ya Lupalilo Ruben Mwandilava amewataka wananchi kutoifuata kauli inayotolewa na uongozi wa Halmashauri hiyo kutokana na wananchi kugawiwa viwanja na kupimwa na Halmashauri yenyewe.
Mwandilava amesema hatua hiyo inawaumiza wananchi na siyo jambo la viongozi kufurahia utekelezaji wa majukumu yanayoikera jamii ambayo ni chachu kuu ya maendeleo.
Hata hivyo mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Makete Imelda Ishuza amesema Halmashauri imeandaa barua kwa maaafisa watendaji wa Kata kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya zoezi hilo.
“Baada ya kusikia taarifa ya wizara tumesitisha zoezi hilo na bado hatujaanza tathmini juu ya malipo ya fidia kwa wananchi watakaokumbwa na zoezi hilo,”Alisema Ishuza.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment