Diwani wa Kata ya Ruiwa,katika Wilaya ya Mbarali Mbeya, bw. Alex Mdimilaje ametoa msaada wa mizani 7 yenye thaani ya zaidi ya shilingi laki 8 kwa vijiji vya kata hiyo ili kuwasaidia akinamama kuwapima watoto wao, hali ambayo hushindwa kuitimiza kutokana na umbali mrefu wa zilipo Zahanati na hivyo watoto kuikosa huduma hiyo.
Mdimilaje amesema mizani hiyo ni moja ya utekerezaji wa ahadi zake katika kampeni wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na kuwataka wananchi hao kumuhoji juu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kila baada ya miezi mitatu.(Robo tatu ya mwaka).
Amesema hali hiyo itamuwezesha kutimiza ahadi zake kwa wananchi na kupunguza kero mbalimbali zinazoikabiri Kata hiyo ya Ruiwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment