Bibi wa kijiji cha Nyeregete katika Mji mdogo wa Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, akitoka kuzagaa kuni na wajukuu zake, ambao ameshindwa kuwapeleka shule kuipata elimu kwa kukosa msaada wa kumuwezesha kufanya hivyo.
Hali hiyo inachangiwa na baadhi ya wakuu wa shule kuwataka wazazi wa wanafunzi kuchangia michango mbalimbali, huku Wakiwafukuza wanafunzi ambao hawakuweza kutimiza masharti hayo.
Michango hiyo ambayo sasa imekuwa kero kwa jamii zenye kipato duni na hata kuiomba serikali, irudishe ada ya shilingi elfu mbili , ambayo waliimudu kwani mpango huo wa awali kila mzazi alifahamu kuwa hilo ni jukumu lake kwa msimu wa mwaka mmoja kuliko hali ilivyo sasa.
Kuiondoa ada hiyo baadhi ya walimu wamebuni mbinu mpya iitwayo michango, ambayo baadhi ya shule wanafunzi huchangia hadi shilingi elfu 70 kwa madai wizara imewaagiza kuwachangisha wazazi ili kujikimu kwa mahitaji mbalimbali, kama chaki, peni za kusahishia Nk. jambo ambalo linawashinda wazazi walio wengi na wanafunzi kushindwa kuhudhulia masomo kwa kukosa fulsa hiyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment