Thursday, April 14, 2011

UBARUKU WATOA SOMO KWA SERIKALI

Serikali imeshauriwa kupunguza kodi katika pemejeo za kilimo ili wakulima waipate kwa gharama wanayoweza kuimudu.

Hayo yamezungumzwa na wakulima wa kikundi cha Ubaruku wakati walipofanya mahojiano na Ebony fm katika Kata hiyo ya Ubaruku.

Patrick Mbigima mkulima wa kijiji cha Mwanavala amesema srikali kama inahitaji kufanikisha kauli mbiu ya kilimo kwana lazima imuwezeshe mkulima kwa kuondoa kodi katika vifaa vya kilimo.

Mbigima amesema wakulima wanashindwa kujikwamua kiuchumi na kuwa na tija, kutokana na kushindwa kumudu gharama za pembejeo za kilimo za kisasa na kuachana na kilimo cha jembe la mkono.

Amesema changamoto nyingine kwao ni kukosekana kwa vipuri vya pawatila, ambapo kifaa hicho baada ya kuharibika mkulima hurudi kutumia jembe la mkono au jembe la kukokotwa na Ng’ombe.


Joseph Matofari amesema licha ya pembejeo hizo kuuzwa bei kubwa lakini kukosekana kwa soko la uhakika kunachangia wakulima kupunjwa na wafanyabiashara kwakati wa mauzo.

Luchana Kiponda amesema pawatila moja kwa sasa huuzwa shilingi milioni kumi (10) wakati awali kifaa hicho kiliuzwa shilingi mil. Tano (5) na hivyo baadhi ya wakulima kuendeleza kilimo cha jembe la mkono ambalo hutumia nguvu na muda mwingi katika eneo dogo.


MWISHO

No comments:

Post a Comment