NJAMA za kumng’oa Mbunge wa jimbo la Mbarali Bw.Bw.Dicksoni Kirufi kupitia chama cha mapinduzi Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya zimeshika kasi baada ya kikao cha Halmashauri kuu ya Wilaya hiyo kuazimia kumnyang’anya kadi ya uanachama mbunge huyo kwa madai ya kuwa amekuwa chanzo cha mgogolo kati ya wananchi na mwekezaji wa shamba la Mbarali Estate.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kumalizika kwa kikao kwa kikao hicho ambacho kilifanyika April mosi mwaka huu ulkiofanyika katika katika ukumbi wa Lutheranin Kata ya Rujewa kuanzia majira ya saa nne hadi saa kumi jioni kujadili namna ya kumnyang’anya kadi ya chama Mbunge huyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya washiriki wa kikao hicho ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini walisema hatua hiyo imefikiwa baada ya shinikizo la mwenyekiti wa CCM wilaya kuwa na mgogolo binafsi na mbunge huyo na kuchukua mamlaka yake kuwashinikiza wajumbe kuingia katika maamuzi hayo.
“Sisi hatuna tatizo na Mbunge wetu lakini mwenyekiti wa wilaya kaamua kuukuza ugomvi wao binafsi kwa kuuleta kwa sisi wajumbe, jambo ambalo hatujawahi kuona, na ni vitu ambavyo havihusiani hata kidogo,”Walisema.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wajumbe hao zilisema kuwa ugomvi huo unatokana na mbuge Kilufi kuwajirani na wananchi ambao wanamgogolo na mwekezaji wa shamba la Mbarali Estate ambako mwenyekiti huyo wa ccm anafanyia kazi.
Wamesema majadiliano hayo yalichukua muda mrefu kumalizika kutokana na pande mbili kutofautiana juu ya maamuzi hayo ambayo yanalenga kumuondolea wadhfa alionao mbunge kwa kumtoa madarakani.
Wamesema kikao hicho kiliwashirikisha baadhi ya wanachama ambao waliandaliwa na mwenyekiti huyo ili kupata nguvu ya kuungwa mkono kwa hoja hiyo.
Hata hivyo Mpango huo unaodaiwa kuandaliwa muda mrefu na mwenyekiti huyo kupinga kupita katika kura za maoni kwa mbunge huyo na kumjengwa chuki ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa mbunge licha ya kuwa kundi kubwa la wananchi na viongozi wa CCM wilayani humo wanamkubali mbunge.
“Sisi Kilufi ni chaguo letu, lakini taratibu zinazotaka kufanyika tunaona zinaweza kutugawa ndani ya CCM, wanasema mbunge anachochea mgogolo wa shamba, wakati si sahihi kabisa kwani taarifa za matukio hayo mgogolo eneo la mwekezaji na wananchi wa Ubaruku mbunge huwa msuluhishi mkubwa hata uongozi wa wilaya unaposhindwa,”.
Wamesema kupitia mpango huo mwenyekiti huyo anataka kuisamabaratisha CCM ndani ya Wilaya hiyo kwa kuwa mbunge huyo ni chaguo la wananchi wengi ingawaje baadhi ya viongozi wa wilaya hawamkubali kwa maslahi yao binafsi.
Hali hiyo imeanza kujitokeza tangu mbunge huyo kujiingiza katika kinyang’anyiro cha nafasi hiyo ambapo asilimi kubwa ya viongozo walikuwa wanampenda mbunge aliyekuwa madarakani Estelina Kilasi, na kuanguka kwa mbunge huyo kulizuka mgawanyiko wa ccm “A” na ccm “B” na hivyo Kilufi kujikuta anaupinzani mkubwa ndani ya chama ambacho kimempa ridhaa ya kuongoza.
Wananchi wa wilaya hiyo wamesema mpango huo endapo utafanikiwa kwa kunyang’anywa Kadi ya uanachama wa CCM Kilufi, Chama hicho kitapoteza mwelekeo na hata jimbo kuchukuliwa na vyama pinzani kutokana na kundi kubwa la wananchi kumkubali mbunge huyo.
Hata hivyo Mbunge huyo alipopigiwa simu yake ya kiganjani alikiri kupata taarifa hizo za kutaka kunyang’anywa kadi ya chama kutoka katika kikao hicho ambapo baadhi ya viongozi walimpa taarifa hizo za shinikizo la maazimio hayo.
“Taarifa hizo nimezipata, lakini tatizo kubwa ni mwenyekiti kuwa na chuki binafsi juu yangu, ni mgogolo wa muda mrefu kwani hata kwenye kampeni zangu hakuwahi kushirii kama mwenyekiti, mimi nilidhani baada ya kumalizika uchaguzi na tofauti hizo zitaisha ili tushirikiane kuleta maendeleo kwa wananchi, lakini hali hiyo imekuwa tofauti na mpaka sasa ananiundia mizengwe na kuhakikisha nafanya kila linalowezekana ili kuniondoa madarakani,”.
Amesema hata aliposhinda katika kura za maoni mwenyekiti aliitisha kikao cha kupinga matokeo hayo na kupeleka mkoani na hata taifa lakini adhma yake haikufanikiwa, na kuuomba uongozi wa chama Taifa kuliangalia kwa makini tatizo hilo ambalo linakua kila kukicha kutokana na kuanzia katika ngazi ya uongozi wa wilaya.
Bw. Kilufi amesema yeye ni mbunge wa wananchi wote na siyo baadhi ya kundi la watu kwa maslahi binafsi na katika migogolo hiyo hausiki kwani yeye kama mbunge ni lazima awasikilize wananchi wanapolalamika na kufanya hivyo kumemfanya aonekane kama anaratibu vurugu hizo.
“Sijawahi kuitwa ili nipewe taarifa za makosa yangu chaman nafahamu changu ni chama makini kina taratibu zake za kimsingi na madhubuti, kama kuniita, kunihoji juu ya ukiukwaji wangu wa maadili, kunionya kwa barua na hata kunipa nafasi ya kujieleza kwa maandishi, ili wanisikilize juu ya utetezi wangu na kama ninamakosa kinaweza kunipa adhabu ya kujirekebisha, lakini hayo yote sijahusishwa na ninasikia tu , hizo ni chuki binafsi za baadhi ya viongozi wa chama hasa mwenyekiti wangu.
Hata hivyo katibu wa CCM wilaya Bw.Mkanyege Kashiririka alipotakiwa kuzungumzia tatizo hilo alisema jambo hilo msemaji ni mwenyekiti wa CCM wilaya Bw. Ignas Mgao ambaye alidai kuwa hana ugomvi wowote na mbunge na kuhusu kutoshiriki katika kampeni alisema katiba ya chama hamruhusu kuingia katika kampeni bali ni sekretarieti ya chama.
Aidha mwandishi wa Blog hii alipomtaka mwenyekiti huyo wa Chama cha mapinduzi kutaja jina lake alisema mtu aliyekupatia namba yang undo akupe jina langu si ndo amekupa namba basi na jina akupe yeye.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment