Kaimu mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Mosses Mashaka akisisitiza wananchi kuacha tabia ya kuishi nyumba moja na wanyama.
Jamii imeshauriwa kuacha mara moja tabia ya kuishi nyumba moja na wanyama ili kuepukana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB)
Rai hiyo imetolewa na kiongozi huyo ambaye ni afisa tawala wa Wilaya ya Mbarali wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu ambayo kiwilaya imefanyika katika kijiji cha Utulo katika Kata ya Mapogolo Mbarali.
Wito huo umetolewa na Bw. Mashaka ambaye ni afisa tawala wa Wilaya ya Mbarali ambaye alikuwa kaimu mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, ambapo amesema hali hiyo inachangia kwa kiwango kikubwa ogezeko la ugonjwa wa TB hasa kwa jamii ya wafugaji.
Wilaya ya Mbarali imefanya maadhimisho hayo tarehe 1-4 mwaka huu badala ya tarehe 24 ya mwezi wa 3 ambayo ni maadhimisho ya siku hiyo kidunia kutokana na ukosefu wa rasilimali.
No comments:
Post a Comment