Wednesday, May 4, 2011

Mwenyekiti amkimbia naibu waziri

Mwenyekiti wa kijiji cha Usuka katika Wilaya ya Njombe Melimeli Kinyaga amelazimika kuukimbia msafara wa naibu waziriambaye ni mbunge wa jimbo la Njombe Magharibi Mh. Injinia Gerson Lwenge wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kumchagua kuwa Mbunge.

Mwenyekiti huyo alilazimika kuchukua jukumu hilo baada ya swananchi kumueleza kuwa wanataraji kutoa taarifa ya kutosomewa mapato na matumizi ya serikali ya kijiji kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Melimeli ambaye alifika katika mkutano huo ambao ulifanyika katika ghala la mazao na baada ya kipindi cha maswali kuamua kukimbia mkutano hupo abapo mbunge Lwenge alimtaka kujibu tuhuma zinazotolewa na wananchi wake na kushuhudia kiti kitupu.

Levi Mhugo alisema mwenyekiti huchangisha michango mbalimbali, ikiwamo la mpango wa utengenezaji wa madawati, ambapo kila mwananchi alitoa debe moja la zao la Alizeti na baada ya hapo hawafahamu lolote juu ya hatma ya mchango huo.



“Mheshimiwa mbunge, sisi tunajuhudi sana katika kuchangia jenzi mbalimbali na shughuli za maendeleo, lakini tunakwamishwa na viongozi wetu hawatusomei fedha zetu zilizopatikana ili tuwe na imani na kuendelea kuchangia tena miradi mingine,” Alisema Mhugo.



Alisema pia katika mpango wa kuboresha sekta ya elimu, kila mwananchi alichangia shilingi elfu mbili kwa ajili ya ujenzi wa shule, lakini fedha hizo hazifahamiki zilipatikana kiasi gain na ziko wapi.



Wananchi hao walisema hivi karibuni mwenyekiti aliwachangisha kila mmoja debe moja la Alizeti kwa madai ya mchango wa kuchonga madawati hayo ili kuwaepusha wanafunzi na adha ya kukaa chini lakini hakuna dawati hata moja lililochongwa na mpaka sasa wanafunzi wanakaa chini.


Ofisa mtendaji wa kijiji cha Usuku Bw. Yohabu Myamba alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia hali hiyo ambayo hata katika mikutano mikuu humtaka mwenyekiti
asome mapato na matumizi ya kijiji chao na kukwamishwa na mahdhulio ya baadhi ya viongozi.

No comments:

Post a Comment