Sunday, January 1, 2012

MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA ALALAMIKIA KUTOPEWA MTOTO WAKE WA KIUME KULWA


  1. Mwanamke Amida Mtundwe (kushoto) ambaye anadaiwa kujifungua watoto mapacha wawili na mmoja kulwa wa kiume kutopewa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali, licha ya kadi yake kuandikwa kuwa amejifungua mapacha. Kulia  aliyemshika mtoto ni mmiliki wa blog hii - Oliver motto alipofika katika kijiji cha Mwakaganga Kata ya Ubaruku Mbarali Mbeya.
  2. KATIKA Hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja Amida Mtundwe, mkazi wa kijiji cha Mwakaganga Ubaruku, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya anadai mtoto wake katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali, baada ya kujifungua mapacha na kupewa mtoto mmoja.

  1. Akizungumzia mkasa huo Amida amesema tangu akiwa mjamzito alipimwa na kuambiwa ana mimba ya watoto wawili (mapacha) na siku ya kujifungua aliambiwa atafanyiwa oparesheni, usiku wahudumu wa Hospitali  ya Wilaya  ya Mbarali walimuita na kumfanyiwa upasuaji, pasipo wazazi wake kujua.


  1. Amesema amefuatilia mtoto huyo bila mafanikio, na baada ya kuanza Clinik katika Hospitali ya misheni Ubaruku, walimtaka arudi Hospitali ya Wilaya ili kupata maelezo ya mtoto mwingine aliko, kwakuwa kadi yake ya maendeleo ya Uzazi iliandikwa amejifungua watoto mapacha wawili.

  1. Naye mume wa Amida Bw. Zuberi Lutanile kabla ya mkewe kwenda Hospitali  alipiga fotocopy kadi hiyo kama ushahidi, ambayo imeandikwa Amida Mtundwe kajifungua kwa oparesheni watoto wawili, kulwa wa kiume na Doto wa kike, lakini wananchi wanasemaje juu ya tukio hilo!!.


  1. Naye mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali Dr. Boniface Kasululu akizungumza kwa njia ya simu mambo yalikuwa hivi ..



                             Mwisho

No comments:

Post a Comment