WANAFUNZI 12 wa shule ya sekondari Mengele, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wamekatisha masomo kwa tatizo la kupata mimba, na kufuta ndoto zao za baadaye, kutokana na kupanga mitaani.
Akizungumza na mmiliki wa mtandao huu shuleni hapo, mkuu wa shule ya sekondari ya Mengele, iliyopo katika Wilaya ya Mbarali Sophia Tarimo amesema moja ya changamoto inayoisumbua shule hiyo ni tatizo la mimba.
Tarmo amesema tatizo hilo linatokana na kukosekana kwa mabweni shuleni hapo, kwani asilimi kubwa ya wanafunzi wanatoka vijiji vya mbali, na hivyo kulazimika kupanga mitaani na kuwa huru kwa kukosa ulinzi.
Hata hivyo wazazi wameitaka serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuunga mkono jitihada za wananchi ili kukamilisha ujenzi wa sekondari ya Ihahi na kupunguza idadi ya wanafunzi kutembea umbali mrefu na baadhi yao kupanga mitaani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment