KAMPUNI ya Serengeti Brewieries inayozalisha vinywaji mbalimbali kama Tusker, Uhuru, The kick, Seringeti nk. imetenga zaidi ya shilingi Milioni 300 ili kuboresha huduma ya maji
katika mkoa wa Iringa.
Akizungumzia mpango huo mbele ya naibu waziri wa maji Gerson Lwenge,wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa kuvuna maji ya mvua katika Hospitali ya Manispaa ya Iringa, ofisa uhusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Tedy Mapunda, amesema kampuni imemeamua kuwekeza katika huduma ya maji kwa jamii.
Tedy amesema kati ya fedha hizo, shilingi milioni 200 mwaka huu wamewekeza katika miradi salama ya maji, ikiwa pamoja na uvunaji wa maji ya mvua katika Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa.
Amesema wameanzisha mpango wa kutoa elimu kwa jamii, ili kuvilinda vyanzo vya maji na miundombinu yake, ikiwa pamoja na kuweka matenki ya lita elfu 60 kwa ajili ya kuvuna maji katika Hospitali hiyo.
Aidha amesema lengo la mpango huo ni kurejesha huduma kwa jamii, kutokana na kampuni hiyo ya Serengeti kutumia huduma ya maji kwa kiwango kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa zake.
Naye Naibu waziri Lwenge amezindua ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji ya mvua, ambalo litagharimu zaidi ya shilingi Milioni 50 zinazotolewa na Kampuni ya Serengeti, huku Milioni 150 zitapelekwa katika Hospitali
ya Seketule Mwanza pamoja na Hospitali ya Mawenzi Kilimanjaro na Dar es salaam katika Hospitalia ya Temeke.
Ofisa uhusiano wa kampuni ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda akieleza malengo ya kampuni kujikita katika masuala ya kuchangia huduma ya maji kwa wananchi, akiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Iringa, Uzinduzi uliofanywa na Naibu waziri wa maji, Mh. Geryson Lwenge.
No comments:
Post a Comment