Friday, May 11, 2012

NAZINGATIA MASOMO KWANZA!!


Asilimia kubwa ya wananchi mkoani Iringa ni wenye kipato kidogo, hali hiyo inachangia hata wanafunzi kushindwa kupata muda wa kujisomea kwa baada ya kutoka shule, hukumbana na shughuli za kiuchumi ambazo baadhi yao hutumwa na wazazi wao, huku wengine wakiwa wanalazimika kufanya biashara hizo kutokana na kutokuwa na wazazi/ walezi wanaowale.

Hali hii ya kiuchumi inawafanya watoto wengi wasio na mwamko wa elimu kuamua kuacha masomo na kujikita katika biashara ili kuyamudu maisha yao ya kila siku, kutokana na kwamba wale wasio na wazazi/ walezi hujilea wenyewe.

 Mwisho


No comments:

Post a Comment