MASIKINI WANAFUNZI HAWA!!
wanafunzi hawa wanachota maji katika mfereji wa maji ya umwagiliaji Mbarali.
WANAFUNZI wa shule ya
msingi Rujewa iliyopo katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya wakitumia mbinu ya
kushikana mikono ili kuchota maji, mbinu ambayo ni hatari zaidi kwa usalama wa maisha yao, kwani mmoja
atakapoachia mkono wa mwenzie wanaweza wakatumbukia.
Wilaya ya Mbarali inakabiliwa na shida ya maji kutokana na
hifadhi ya Mpanga Kipengele kuzuia Halmashauri kutoendeleza mpango wa ujenzi wa
huduma ya maji katika eneo hilo
ambalo ni poli la akiba lililopo katika Mkoa wa Njombe na Mbeya katika Wilaya
ya Mbarali.
No comments:
Post a Comment