Tuesday, May 22, 2012

WANAHABARI WAPATIWA ELIMU YA UANDISHI WA HABARI ZA BIASHARA NA UCHUMI






Mwezeshaji wa mafunzo ya habari za biashara na uchumi Bw. Mnaku Mbani akitoa maelezo juu ya uandishi wa habari za Biashara na uchumu, mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Maktaba manispaa ya Iringa.


WAANDISHI wa habari mkoa wa Iringa wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuifanya jamii kuelewa taifa linakoelekea.

Akitoa elimu hiyo,  muwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Mnaku Mbani amesema lengo la semina hiyo ni katika kuwanoa wanahabari nchini kuwa na uelewa katika masuala ya uchumi.

Mbani amesema hatua hiyo ni kutokana na waandhishi wengi kutojikita katika uandishi huo wa habari za biashara na uchumi na hivyo eneo hilo kutotendewa haki.

 Mwandishi wa habari mkongwe mkoni Iringa, Bw. FullJeans Malangalila akifuatilia mafunzo hayo ya biashara na uchumi.


Mwanahabari wa radio Ebony fm  Allen Phillip akiendelea na darasa la uandishi wa habari za biashara na uchumi.
 

No comments:

Post a Comment