Monday, June 4, 2012

CHADEMA WATOA ONYO KWA MWEKEZAJI




CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kimetoa onyo kali kwa mwekezaji wa shamba la Mbarali Estate lililopo katika Wilaya hiyo kwa madai ya kutumia shamba hilo kisiasa.

Tamko hilo limetolewa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbarali Peter Mwashiti katika viwanja vya mikutano Kata ya Ubaruku wakati wa mkutano wa chama hicho na kuwa mwekezaji huyo anatumia vibaya shamba hilo la serikali ambalo ni mali ya wananchi wote, kwa kuigawa jamii ya watanzania

Naye ofisa mahusiano wa shamba hilo la mwekezaji la Mbarali Estate Bw. Ingas Mgao alikataa kuhusika na tuhuma hizo huku akigoma kuelezea undani wa tuhuma hizo zinazoikabili kampuni hiyo.

CHADEMA kinataraji kufanya mkutano katika viwanja hivyo vya Ubaruku siku ya jumapili, kwa lengo la kupinga tabia hiyo na kutoa tamko juu ya madai mbalimbali yanayotokea katika Wilaya hiyo, mkutano unaodaiwa kuhudhuliwa na viongozi wa ngazi za juu.
                                                        



No comments:

Post a Comment