Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chale cha Grand Malt imetoa fedha kwa washindi wa shindano la "EXCEL WITH GRAND MALT COLLEGE" imekabidhi zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa wanafunzi wa chuo kishiriki cha Tumaini na Ruaha (TUCO).
Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Iringa Bw. Reymond Degera akitangaza majina ya washindi
Meneja mauzo wa kampuni ya TBL mkoa wa Iringa Bw. Reymond Degera akitangaza majina ya washindi wa shindano la "EXCEL WITH GRAND MALT COLLEGE" wakati droo hiyo ilipochezeshwa katika chuo cha Tumaini mkoani Iringa, ambapo zaidi ya shilingi Milioni 10 ziklitolewa kwa wanafunzi wa chuo cha Tumaini na Ruco.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo akishangilia kuingia katika droo ya shindano hilo, lililofanyika katika viwanja vya mpira katika chuo kikuu cha Tumaini Mjini Iringa.
Msanii wa muziki wa Bongoflever Fid Q- akitumbuiza wanafunzi katika uwanja wa Chuo kikuu cha Tumaini.
Viongozi wa kampuni ya TBL na kinywaji cha Grand Malt wakiwa katika meza kuu, wakibadilishana mawazo katika droo ya kumpata mshindi wa shindano la Excel With Gerand Malt College.
No comments:
Post a Comment