Msanii wa maigizo Leila wa kikundi cha Mzizi cultural Group akimkabidhi mtoto mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa, Bi. Teresia Mahongo, wakati akitoa ujumbe wa kuhusu maisha ya wasichana wenye watoto na maisha magumu kama ni moja ya elimu ya mradi wa "Afya ya uzazi ni haki ya kijana Tuitetee"
Watoto wakisoma kijarida kama walivyokutwa na camera hii, katika kiwanja cha Mwembetogwa wakati wa kongamano la vijana kupitia "Afya ya uzazi ni haki ya kijana, Tuitetee"
Kikundi cha Sanaa, kikitoa burudani kwa wananchi waliofika katika uwanja wa Mwembetogwa, katika kongamano la Vijana, kupitia kaulimbiu ya "Afya ya Uzazi ni haki ya kijana Tuitetee!!".
Vijana wakisoma vitabu katika moja ya banda lililoandaliwa katika kongamano la vijana, mjini Iringa.
Jukwaani ni Msanii wa kizazi kipya, Sqeeezer akiwa na muimbaji wake Malselina, wakitumbuiza katika kongamano la vijana, katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.
Shirika la AMREF kupitia mradi wa "Afya ya Uzazi wa vijana" imefanya kongamano la Vijana katika Manispaa ya Iringa, kwa lengo la kutoa elimu kwa kundi hilo ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ya kujihusisha katika matumizi ya dawa za kulevya, ngono zembe zinazosababisha, mimba kwa wasichana, magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
No comments:
Post a Comment