Katika mazingira ya kutatanisha aliyewahi kuwa mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa Bwana Makosa aliyetangaza kujinyonga katika tukio ambalo alidai atalifanya hadharani na atayetaka kushuhudia atalipia kiingilio ambacho kwa mujibu wake kingesaidia familia yake na watoto yatima.
Mwananchi huyo ameahirisha kufanya tukio hilo, na kuwa hafikirii kama kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za jamhuri na hata katika vitabu vya dini jambo hilo ni dhambi kubwa maana mwenye mamlaka juu ya kuchukua uhai wa mtu ni yule aliyetoa uhai ambaye sote tunaamini ni Mungu mmoja aliye juu mbinguni.
Sasa kwanini Makosa ameamua kufanya hivi??? ifuatayo ni Execlusive Interview fupi kati ya blog hii na Makosa.
Mdau:Je ni lini unatarajia kutimiza lengo lako la kutaka kijinyonga?
Makosa: Embu nichukulie kiroba kwanza
Mdau: Kwahiyo nikikununulia kiroba kitakuwa ndio kiingilio changu siku ambayo utajinyonga?
Makosa:Sijinyongiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mdau: Kwahiyo umehairisha zoezi la kujinyonga ?
Makosa:Sijinyongiiiiiii.
Baada ya hapo makosa akaanza kinipa Free style yaani alikuwa ananiimbia nyimbo anayotaka kwenda kuirekodi hivyo akaniomba ushauri ni studio gani anaweza kwenda.
Mdau: Nadhani kwa jinsi unavyoimba ukienda kwa Marco Chali ataitendea haki nyimbo yako.
Nikamwambia kama anaweza kuimba kidogo labda naweza kuwa meneja wake nikivutiwa na kipaji chake
Pata ladha ya mistari ya wimbo wa Makosa.
Makosa: "Watoto wangu wana miiili midogo dogo ila wana Sauti" KUBWAAA, mke wangu anamwili mdogo mdogo mdogo ila ana matatizo makubwa, Toka siku nyingi mimi marafiki zangu ni watu "WAKUBWAA.
Mdau: Inatosha inatosha nimekubali kweli we ni mtu mkubwaaa ha ha ha ha
Wadau wa blog hii hiyo ilikuwa execlusive interview kati yangu na Jamaa aliyetangaza kujinyonga kwa kiingilio je mdau unaweza kumuweka katika kundi gani?
Mahojiano haya nikwa niaba ya mwenyekiti Majjid Mjengwa.
No comments:
Post a Comment