Thursday, July 26, 2012

KITCHEN PARTY YA ROSEMARY NASARY WA MAFINGA IRINGA

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KWA ROSEMARY NASARY

Bi. Rosemary Nasary, bibi harusi mtarajiwa, akiwa katika pozi, ndani ya ukumbi wa BP. Kangesa wa mjini Mafinga, mkoani Iringa.


Bi. Rosemary Nasary akiwa na mpambe wake usiku wa Kitchen party.


Akiwa na mpambe wake, akiangaliwa kama katoka chicha.

Mama mzazi wa Rosemary Nasary- akiwashukuru akinamama wa mji wa Mafinga, kwa kuandaa sherehe ya mwanae.

Dada wa Rosemary akitoa nasaha kwa mdogo wake, namna ya kuishi na walimwengu.

Bibi wa Rosemary akitoa mafunzo kwa mjukuu wake

Shangazi mtu naye hakuwa nyuma, hapa anatoa usia kwa anti (Shangazi) yake, juu ya uvumilivu ndani ya nyumba.

Rafiki huyu naye akaona anayo machache ya kumsisitizia Rosemary, kuhusu usafi, yupo vizuri. 

"Na mimi nina mchango wangu, Rosemary kuwa makini na marafiki,"

Mmoja wa washiriki kijisosomoa kwa vyuku na vinywaji.


Wataalamu waliobobea katika shughuli za usasambuaji , wakiwa kazini.


ZAWADI MBALIMBALI ZILITOLEWA, KAMA KITANDA, KABATI LA NGUO LA VYOMBO NA VYOMBO VYAKE VYOTE VYA NYUMBANI 



Zawadi ya Kitanda 
Kabati la vyombo na baadhi ya vyombo vya mfano.



Mc. Salome, akifanya mambo yake katika kusherehesha tafrija hiyo.





Imefanyika katika ukumbi wa BP. Kangesa katika mji wa Mafinga mkoani Iringa.

MTANDAO HUU UNAMTAKIA AFYA NJEMA ROSEMARY, PAMOJA NA FAMILIA NZIMA KATIKA KUFANIKISHA SHEREHE YA HARUSI.

No comments:

Post a Comment