Sunday, July 1, 2012

MWENGA KUWASHA UMEME WAKE MWEZI HUU WA 7 NA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI IRINGA




Bango la Umeme wa Mwenga, katika kijiji cha Isipii, unaotarijia kuwaka mwezi wa 7 na  kuleta maendeleo kwa wananchi Wilayani Mufindi, mkoani Iringa, ambao umejengwa kwa ufadhili wa jumuiya ya Ulaya EU.


Fundi akiendelea na kazi ya kufunga mitambo kwa ajili ya kufanya ukamilisho wa mradi huo.

Fundi akiendelea na kazi ya kufunga bomba kubwa la chuma (Penstock) ambalo hupitisha maporomoko ya maji kutoka katika chanzo na kupeleka katika jengo la ufuaji wa umeme.

Mkurugenzi mpya wa taasisi ya utafiti wa chai nchini (Tea Research Institute of Tanzania) Bw. Emmanuel Simbua, akitoa ufafanua juu ya mradi huo na fedha zilizotolewa na jumuiya ya Ulaya- EU, ndani ya jengo la kufulia nishati ya umeme.


Meneja wa mradi wa umeme wa MWENGA HYDRO POWER  Michael Gratwicke akitoa taarifa ya mradi kwa ofisa uhusiano wa Ubarozi wa EU Bw. Emmanuely Kihaule, (Pichani hayupo) aliyeongozana na jopo la wanahabari nchini katika kukagua miradi iliyofdhiliwa na jumuiya hiyo ya Ulaya.



UMEME wa Mwenga Hydro Power uliojengwa kwa ufadhili wa jumuiya ya Ulaya EU, kwa lengo la kukomboa maisha ya wananchi waishio vijijini, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa unataraji kuwashwa hivi karibuni baada ya baadhi ya miundombinu yake kukamilika.

Hayo yamezungumzwa na meneja wa mradi huo Michael Gratwicke alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa ofisa uhusiano wa Ubarozi wa EU Bw. Emmanuely Kihaule, akiongozana na jopo la wanahabari nchini, ambapo Grtwicke alisema kuchelewa kwa mradi huo kuanza kumechangiwa na  ugumu wa usafirishaji wa mabomba makubwa ya chuma (Penstock) ambayo hupitisha maporomoko ya maji kutoka katika chanzo na kupeleka katika jengo la ufuaji wa umeme.

Gratwicke alisema hali hiyo iliwafanya mafundi kusubiri vifaa kwa muda mrefu, wakati wa mvua , wakisubiri  zipungue kunyesha ili kuruhusu magari hayo kupeleka mitambo katika eneo la kazi, na hivyo kuwepo kwa ugumu wa shughuli hiyo, na sasa Umeme unataraji kuwaka mapema mwezi wa 7 mwaka huu wa 2012, ambapo vijiji 14 vilivyopo jirani na mradi huo vitanufaika na nishati hiyo.







No comments:

Post a Comment