Sunday, August 26, 2012

PROFF: MSOLLA ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA WALEMAVU


Proff- Peter Msolla akisalimia na watoto wenye ulemavu katika kituo cha "Kijiji cha Walemavu" Kituo hicho kinalea watoto yatima na walemavu wa aina zote, wakiwemo wenye mtindio wa ubongo.

Mkurugenzi wa kituo cha "Kijiji cha Walemavu" Paroko Philip Mamano(aliyemnyanyua mtoto) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Bw. Mohmed Gwalima.

 Proff: Peter Msolla, ambaye ni mbunge wa jimbo la Kilolo akiwa na mkurugenzi wa kituo, paroko Mamno, wakijadiliana juu ya watoto hao.

Proff: Msolla akiwatazama watoto hao ambao kwa mujibu wa uongozi wa kituo, familia zao zimewatelekeza.


Proffesa Msolla akionyesha kitu, wakati akifanya mazungumzo na baadhi ya watoto hao, baada ya kuwatembelea kituoni hapo kama ni moja ya njia ya kuwapa faraja.


Baada ya kuwatembelea watoto, Profesa Msolla aliwatunukia vyeti vya uhitimu wa mafunzo ya elimu ya Astashahada, wahitimu wa 44 wa chuo cha kilimo cha Mtakatifu Maria Goretti,  mbacho ni moja ya kituo cha watoto, kilichopo chini ya Kanisa Kathoriki na kimekuwa kikiongozwa na mkuu wa chuo Paroko Mamano.






No comments:

Post a Comment