Mbunge wa jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) akiwahutubia wananchi waliofioka katika mkutano wake, uliofanyika katika Soko kuu, nje ya kituo cha Polisi mjini Iringa.
Waandamanaji (Waandishi wa habri) wakiwa na moja ya picha za marehemu Daud Mwangosi,wakipinga vikali mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la Polisi, wakati CHADEMA wakifungua matawi yake katika kijiji cha Nyololo Mufindi, mkoani Iringa, ambapo marehemu alikuwa akitekereza wajibu wake wa kuihabarisha jamii.
Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango yenye jumbe tofauti, wakati wa kupinga mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi.
Baadhi ya wananchi manispaa ya Iringa wakisikilima mkutano nje ya Soko kuu mjini Iringa
Baadhi ya wananchi wa wakereketwa wa CHADEMA wakionyesha ishara ya ngumi, wakiwa katika mkutano huo nje ya Soko kuu katika mkutano na mbunge Msigwa.
Mbunge wa Iringa,mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA,jioni ya leo amehutubia umati mkubwa wa wakazi wa Iringa, Katika hotuba yake, Msigwa amesema kuwa hayati Daud Mwangosi ni shujaa ambae atakumbukwa daima.
Tutawaleteeni habari zaidi.
No comments:
Post a Comment