Wednesday, September 26, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI TENA MAHAKAMANI KWA MBWEMBWE, AFIKISHWA KWA GARI LINGINE LA KIFAHARI- AVAA MIWANI HADI NDANI YA MAHAKAMA









Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi  leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.
Akisomewa shitaka lake na  mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Lilian Ngilangwa , alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitaka la mauaji ya makusudi.
Alisema mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5 (a) i cha makosa ya jinai.

Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Wilaya Dyness Lyimo alisema mtuhumumiwa hatatakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuendesha kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.
Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 10 Oktoba  mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jamba ambalo limewaletea ugumu kwa mara ya pili waandishi wa habari waliokuwapo katika mhakama hiyo kwani walisukumwa na kuzuia kumpiga picha mtuhumiwa huyo, huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuvaa miwani mieusi kuhakikisha kuwa sura yake haionekani.

Lakini jambo la kushangaza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili DFP 2175 Toyota Land cruiser tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi(Karandinga), gari hiyo ikiwa tofauti na ile ya awali ambayo ilikuwa namba T 320 ARC ambapo pia alivalia kodi kubwa jeusi refu huku kichwani akiwa amejifunika kwa kitambaa kwa ulinzi mkali wa maofisa wa jeshi la
polisi.

Ambapo mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, mkoa wa Iringa Michael Luena alisema kesi hiyo namba 01.RM ya mauaji kifungu namba 196, ipo chini ya kanuni za adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2012.

Luena  alisema mtuhumiwa huyo mwenye namba G. 2573  Pasificus Creophace Simion 23,  kabila Muhaya na mkazi wa FFU anatuhumiwa kwa kosa la mauaji (Mada) ambapo  alitenda kosa hilo katika kijiji cha
Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, siku ya tarehe 2 ya mwezi wa tisa (Septemba) 2012, kwa kumuua Daud Mwangosi.

Mtuhumiwa pia hakutakiwa kujibu lolote, kutokana na mahakma hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendesha  kesi za mauaji na hivyo hakimu Dyness kuamuru mtuhumiwa apelekwe magereza hadi tena kesi hiyo itakapotajwa tena tarehe 26 mwezi wa tisa, kutokana na kesi yake kutokuwa na dhamana.

Ambapo msaada wa wanasheria mahakamani hapo, walisema kesi hiyo ya mada ina maana ya kuua kwa kukusudia na uendeshaji wa kesi hizo una hatua nyingi hadi ushahidi ukamilike , ambapo mtuhumiwa hatakuwa na uwezo wa kujibu chochote katika ngazi ya mahakama hiyo.

“Kesi hii ya mada ina mana aliua kwa kukusudia, ndiyo maana dhamana yake imezuiliwa, lakini ingekuwa ya kuua bila kukusiudia dhamana yake ingekuwa wazi,” Alieleza mmoja wa wanasheria wa mahakama hiyo.

Alisema hatua hiyo inatokna na kifungu cha 148 kifungu cha 5 - "a" 1 (Roman One)  ambacho kinazuia dhamana kwa baadhi ya makosa ikiwemo kosa la mauaji ya kukusudia.

Walisema kifungu hicho kinamnyima dhamana mtuhumiwa na anatakiwa kwenda Magereza ambapo sasa ni mahabusu hadi kesi yake upelelezi wake utakapokamilika.
                                                             MWISHO

No comments:

Post a Comment