Thursday, May 9, 2013

DC GUNINITA APOKEWA KWA SHANGWE NA ALIOWASWEKWA LUMANDE -AMALIZA MGOGOLO


 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mlafu kilichopo tarafa ya Mazombe Wilaya ya Kilolo wakimsikiliza mkuu wa Wilaya hiyo Gerlad Guninita, alipofika kutatua mgogolo wa ardhi unaowakabiri wananchi hao.
 "Tupo makini sana mkuu, ni kma wanasema hivyo wananchi wa Mlafu.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita akizungumza katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Mlafu.
Diwani wa Kata ya Mlafu akikabidhi zawadi ya Mkungu wa Ndizi kwa DC-Guninita. 
 Mwananchi wa kijiji cha Mlafu akikabidhi zawadi.
Mwananchi (Kilungu) akikabidhi zawadi kama ishara ya furaha yake baada ya mkuu huyo kumaliza mgogolo unaowasumbua kwa zaidi ya mika 5. 
Mjumbe wa serikali ya kijiji akikabidhi naye zawadi.
 Mmiliki wa eneo hilo ambalo kisheria aliuziwa ndivyo sivyo (mwenye koti la Kijani) Kiyenge akitoa maneno ya kukabidhi ardhi hiyo mbele ya mkuu wa Wilaya.
 Mazungumzo katika shamba la Mahindi zaidi ya ekari 5, shamba  ambalo limenusulika kuvunwa na wananchi, na hivyo kukemewa na mkuu wa Wilaya kutofanya uharibifu huo.
Ofisa Wilayani Kilolo, akiambatana na msafara, ambao nyumba yake ni mwekezaji wa ardhi Kiyenge akiwa na mpambe wake Kilungu, baada ya kukabidhi ardhi mikononi mwa serikali ya kijiji cha Mlafu.

HATIMAYE mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Gerlad Guninita ambaye siku za hivi karibuni aliwaweka Lumande watumishi wa Halmashauri hiyo ya Kilolo, amemaliza mgogolo uliokuwa unawakabili wananchi wa kijiji cha Mlafu kwa zaidi ya miaka mitano.

Lakini cha kushangaza ni pale mkuu huyo Guninita alipopokewa kwa shangwe, Nderemo na Vifijo baada ya maofisa hao kuandaa vilivyo mapokezi ya mkuu huyo, zikiwemo ngoma za jadi, Vyakula Zawadi mbalimbali pamoja na mapokezi ya aina yake.

Uwepo wa idadi kubwa ya wananchi waliofika katika mkutano huo pia uliwashangaza hata viongozi na wananchi wenyewe na kudai kuwa hali hiyo haijawahi kutokea na nihistoria katika kijiji hicho.

Guninita katika mkutano huo pia aliandaliwa Nyimbo na mashairi yenye jumbe mbalimbali ikiwa ni zawadi na furaha ya ujio wake wa awamu nyingine, na kubwa likiwa ni wananchi kufurahia hatua ya kiongozi huo wa Wilaya kukomalia utatuzi wa mgogolo huo.

Aidha Guninita alifanikiwa kumaliza mgogolo huo ambao kwa mujibu wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mlafu, wametumia gharama kubwa katika kufuatilia mgogolo huo Halmashauri ya Wilaya hiyo pasipo na mafanikio kwa zaidi ya miaka mitano.

Pia mkuu huyo alisema kuna kila haja wataalamu wakatoa elimu kwa wananchi juu ya ardhi ili kutambua sheria zinazowataka katika utoaji wa ardhi za kijiji, kwani serikali ya kijiji haina uwezo wa kutoa ardhi zaidi ya ekari 50 kwa mtu mmoja.

Akitaka ufafanuzi zaidi juu ya ardhi hiyo iliyorudishwa mikononi mwao, mwananchi Elia Muhema alitaka kufahamu juu ya mazao yaliyokuwepo katika shamba hilo, ambapo mkuu huyo aliwataka wananchi wamuache mwekezaji huyo aondoe mazao yake (Mahindi) ili kuendeleza  upendo na mshikamano baina yao.

“Kama kuna mazao jamani hayo mazao ni mali yake, mumuache avune Mahindi yake, nadhani hadi mwezi wa saba atakuwa tayari ameyaondoa,” Alisema Guninita.

Mzee Elias Msola alimpongeza mkuu huyo kwa jitiohada zake za kumaliza mgogolo huo, huku mwekezaji Kiyenge naye akishukuru kwa hatua ya kiongozi huo, ambapo msafara mzima na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji hicho cha Mlafu ulifunga safari hadi katika eneo hilo lenye mgogolo.

Kiyenge alisema awali alihofia mazao yake kutaifishwa na wananchi hao, jambo lililomkosesha amani, na kuwa uamuzi wa mkuu huyo umezingatia haki, na kuwa ardhi hiyo ameirudisha kwa amani na atafuata taratibu za kisheria ili kupata kiwango sahihi kinachotakiwa.

Hata hivyo furaha ya wananchi hao na viongozi wa serikali ya kijiji haikuishia hapo, kwani maandalizi makubwa ya chakula yalifanyika, huku wale viongozi waliowekwa Lumande katika kituo cha Polisi cha Mbigili kilichopo tarafa ya Mazombe wakionyesha furaha tofauti na hisia za wengi walivyodhani. 

No comments:

Post a Comment