Wananchi wakionja adha ya kukosekana kwa usafiri wa daladala.
Wengine walilazimika kutumia Bajaji, wengine Bodaboda, wengine Baiskeri, wengine kwa miguu, ili mradi kupunguza amwendo wa mahali wanakokwenda, ili mradi wafike.
Bango la SUMATRA Mkoa wa Iringa.
Diwani wa Kata ya Miyomboni Kitanzini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akiongoza msafara wa madereva na makondakta kuelekea katika mkutano dharula kujadili utata huo.
Madereva na makondakta wakiwa katika mkutano wa dharula, katika ukumbi wa Hollfea Kitanzini, mkutano ulioandaliwa na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabara mkoa wa Iringa Salm Abri Asas akifafanua baadhi ya mambo ktk mkutano huo.
Wakiwa katika ukumbi huo wa mkutano.
Dereva Best Nazareno akitoa dukuduku lake juu ya ofisa wa Sumatra mkoa wa Iringa.
Dereva akilalamikia manyanyaso ya ofisa huyo.
Dereva akisisitiza jambo kwa kamati juu ya vitendo wanavyofanyiwa na ofisa huyo wa Sumatra.
Baadhi ya Risiti ambazo zimekuwa zikitolewa na ofisa huyo, kosa la kutovaa sare faini laki mbili na nusu.
Risiti ikionyesha tozo la laki mbili kwa dereva wa daladala ya Kalenga Kihesa Kilolo manispaa ya Iringa.
Ofisa Rahimu Kondo akitakiwa kutoa ufafanuzi wa faini alizotoza, (Kulia ni Jesca Msambatavangu diwani kata ya Kitanzini/Miyomboni na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akishangaa.
Mkuu wa polisi mkoa kitengo cha usalama barabarani (RTO) Pamphil Honono akiteta jambo na mwenyekiti wa kamati ya Usalama barabarani Salim Abri Asas, katika mkutano huo.
Ofisa wa SUMATRA hapo shughuli ni pevu kwake, inamlazimu kukiri mapungufu katika utendaji wake wa kazi, ikiwemo matumizi ya Lugha zisizo za STAHA.
Mkuu wa polisi mkoa kitengo cha usalama barabarani (rto) Pamphil Honono akiahidi kushirikiana na madereva na makondakta hao kutatua changamoto zinazowakabiri, kwa lengo la kuboresha kazi na mazingira salama ya shughuli za usafiri na usafirishaji.
KATIKA hali isiyo ya kawaida, madereva wa Manispaa ya Iringa wamemtia akili ofisa wa mamlaka ya usafiri wa majini na nchin kavu SUMATRA kwa kufichua uovu wake aliokuwa akiufanya dhidi ya madereva na makondakta hao wa Daladala.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya madereva na makondakta wa daladala zinazofanyakazi katika Manispaa ya Iringa kufikia muafaka wa kugoma kutoa huduma hiyo, kwa kile walichosema wamechoshwa na uonevu wa ofisa huyo.
Mgomo huo ambao ulianza leo majira ya saa moja asubuhi umeweza kuathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi baada ya wananchi kukosa huduma ya usafiri wa kuelekea katika majukumu yao ya kila siku.
Mgomo huo ulipelekea wananchi kutumia usafiri mbadala wa
Pikipiki almaarufu Bodaboda, Bajaj, na wengine wakiingia gharama ya kukodi Taxi,
baada ya madereva hao kugoma kutoa huduma hiyo kwa madai mengine ya kukataliwa
kuingia katika kituo cha daladala cha
Miyomboni.
Sephania Rajab kondakta wa daladala
za Miyomboni alisema wamekuwa wakitozwa faini kubwa kuanzia shilingi Laki
mbili, hadi laki mbili na nusu, jambo linalosababisha wao kushindwa kupata
chochote katika biashara hiyo.
Naye Bisheni Mgilangwa alisema wapo radhi kulala na njaa endapo
serikali ya mkoa haitamuondoa ofisa huyo wa Sumatra mkoani hapo, kwani amekuwa
akiwanyanyasa na kuwapiga faini ya kuwakomoa.
Issa Gideon alisema licha ya kutozwa
faini hizo pia wamekuwa wakizuiliwa kupakia abiria katika kituo cha mabasi cha
Miyomboni jambo linalowafanya wakose fedha za kurejesha kwa wenye magar.
Issa alisema kutokana na jiografia
ya manispaa ya Iringa inawawia vigumu kutosubiri abiria, kwani hakuna wasafiri
wanaokaa eneo moja zaidi ya kituo cha Miyomboni, ambapo napo tayari wameambiwa
hakuna kuingia.
Kaloli Wilbat alisema pia manispaa
wamekuwa wakiwatoza ushuru mkubwa wa shilingi elfu moja, licha ya kuwa vituo
vya daladala havina huduma yoyote hata ya choo jambo linalowafanya watumie
gharama nyingine katika kupata huduma hiyo muhimu, na kuitaka Manispaa
iwaonyeshe kituo halali cha daladala.
NEEMA Mdoe abiria alisema amelazimika kuchangia
Bajaji shilingi elfu mbili, kutoka Mkimbizi hadi Posta jambo ambalo limempa
hasara kwani umbali huo kwa usafiri wa daladala hutozwa shilingi mia nne.
Naye Hilda Sade amesema amelazimika
kuchelewa kumpeleka mtoto Hospitali baada ya kusubiri muda mrefu bila mafanikio
usafiri wa daladala na kasha kuamua kuchangia shilingi elfu moja ili kupanda
Bajaji.
Hatua hiyo ambayo ilikuwa ikielekea kuathiri uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa iliilazimu kamati ya
usalama barabarani chini ya mwenyekiti
wa kamati hiyo mkoa wa Iringa Salim Abri
Asas, kuwaomba madereva hao kukaa katika meza ya pamoja ili kuyajadili
mapungufu hayo na kuyafanyia kazi.
Katika mkutano huo madereva na makondakta walizungumza masuala mbalimbali likiwemo la ofisa huyo kuchukua fedha hata nyakati za usiku pasipo kutoa lisiti ya makosa husika jambo lililoifanya kamati hiyo kukusanya lisiti nyingine ambazo zilionyesha kughushiwa.
Madereva hao walimtaka ofisa huyo kuwaomba radhi kwa yale yote aliyoyafanya ya kukiuka taratibu za kuishi vyema na wananchi, kwani walisema amekuwa akitumia hata lugha zisizofaa ikiwemo kuwaita madereva kuwa ni "MAHOUSE GIRLS" na huku akijisifu kuwa yeye ni mtoto wa Dar es salaam hawawezi kumfanya lolote.
Katika kufika makubaliano Salim Abri
alisema kuna kila sababu ya madereva wakaheshimiwa kama idara nyingine, kwani huo ni mgawanytiko wa kazi na kuwataka washiriki katika vikao vya kamati ya
usalama barabara ili kubaini mapema changamoto zinazowakabiri.
“Niwaahidi katika hili ndani ya
Kamati yetu ya usalama barabarani, mnatakiwa na nyinyi madereva muwe na
wawakirishi wenu humu, ili tunapojadili baadhi ya masuala pia tupate kero zenu
kupitia wawakirishi wenu,” alisema.
Aidha ameitaka SUMATRA pamoja na jeshi
la polisi kuwa na lugha nzuri Kwa madereva pamoja na makondakTta ili kufanya
kazi kwa ushirikiano na upendo.
“Hapa niwaombe ndugu zangu wa Sumatra
na Polisi, mnatakiwa kuwa na lugha ya Staha, acheni kabisa kutumia lugha za
matusi, haifai hata kidogo,” Alisema Salim.
Mkuu wa polisi mkoa kitengo cha
usalama barabarani Pamphil Honono amewaomba madereva hao kurudisha huduma ya usafiri wa daladala, huku akiwaahidi kushughulikia
kero zote zinazowakabiri madereva na makondakta hao.
Hata hivyo ofisa mfawidhi huyo wa
Sumatra Mkoa aliyekuwa akielekezewa shutuma hizo ..Rahim Kondo aliomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya likiwemo la kuwaita madereva "HOUSE GIRL", kuchana Stika za magari na kisha kuwatoza tena faini ya kutokuwa na kielelezo
hicho, ambapo aliahidi kuzifanyia marekebisho tuhuma zilizomkabili, hatua
iliyopokelewa kwa mikono miwili na madereva na makonda na kuahidia kurejesha tena huduma hiyo muhimu ya Usafiri.
Huduma hiyo ilisitishwa kwa zaidi
ya masaa tisa, kutoka saa moja asubuhi hadi majira ya saa tisa arasili baada ya
mkutano huo, ambao baadhi ya viongozi walikutwa na makosa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment