Mwanamke - anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa.
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.
JESHI la polisi mkoa wa
Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia
mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa
amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.
Wanjiru ambaye ni raia
wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini
kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala ambayo
ni msingi wa utawa wao.
Akizungumzia mkasa huo,
kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke
huyo kabila laKe ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
Aidha Kamuhanda amesema
mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake
nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni
mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.
Kamuhanda amesema Sister
huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja
ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa
na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.
Amesema Sister huyo feki
katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na
nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo FEKI amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
Sister huyo FEKI amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
Kamuhanda ameitaka jamii
kuwa makini na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu
kwa muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya
kila mtu kumuamini.
>>>>>>Katika tukio lingine
jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikiria mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya
Iringa kwa tuhuma za kuiba vielelezo vya madawa ya kulevya aina ya bangi.
Kamuhanda amesema tukio
hilo limefanyika tarehe 14 ambapo mtuhumiwa huyo wa mahakama Lwitiko
Lusekelo Minga ambaye ni mlinzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, aliiba bangi
yenye uzito wa kg 371.2
“Tukio la kupatikana kwa
bangi, eneo la Flerimo mtuhumiwa Juma Nzowa alikamatwa na bangi na baada ya
kuhojiwa mtuhumiwa alimtaja Lwitiko Lusekelo Minga Mlinzi wa Mahakama kuwa
ndiye aliyemuuzia kielelezo hicho cha mahakama,” Alisema Kamuhanda.
Pia amesema kielelezo
hicho awali kilikamatwa Wilaya ya Kilolo na kufikishwa mahakamani kama ushahidi
na ndipo ilipoibiwa tena.
Amesema kutokana na
uwepo wa watumishi wasio waaminifu kumekuwa na tabia hiyo hasa kwa madawa hayo
ya kulevya, vielelezo vyake na kurudi tena mitaani huku wao wakiendelea na
zoezi la kukamata.
Hata hivyo kumekuwa na
malalamiko mbalimbali juu ya vielelezo hivyo kuibiwa pindi vifikapo Mahakamani,
hasa kwa vidhibiti hivyo vya madawa ya kulevya na vipodozi mbalimbali
ambapo huuzwa katika maduka na wananchi kuendelea kutumia.
Aidha vielelezo kama
vyombo vya thamani navyo vimesemekana mara nyingi hupotelea Mahakamani na hata
katika vituo vya Polisi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment