Thursday, May 16, 2013

MAHAKAMA YARUKA KIMANGA KUHUSIKA NA WIZI WA BANGI YA KIDHIBITI


Wanahabari wakiwa nje ya jengo la Mahakama kuu Iringa, baada ya kuitwa na Mahakimu kukanusha taarifa za Bangi ambayo ni kidhibiti cha kesi mahakamani hapo kuibiwa n ammoja wa mtumishi wa mahakam na kuiuza.
 Wanahabari wakichukua maelezo ya Mhe. hakimu Godfrey Ntemi Isaya, ambaye ni kaimu msajili wa mahakama Wilaya ya Iringa, wakati akikanusha taarifa ya mahakama yake kuyibiwa Bangi.
 Mhe. Hakimu Godfrey Ntemi Isaya, kaimu msajili wa mahakama Wilaya ya Iringa, akisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari.
 Baadhi ya mahakimu wakiwa katika kikao hicho cha kukanusha tuhuma za bangi ambayo ni kielelezo kuibiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa.

 Kikao kinaendelea.
" Ndani ya kikao cha dharula".
 Wanahabari wakiwa katika ofisi ya mahakama katika kikao hicho cha dharula.
 Wanahabari wakionyeshwa Guba la kuchomea madawa ya kulevya na baadhi ya takataka, eneo ambalo linadaiwa bangi hiyo iliteketezwa hapo.
 Mahakimu wa mahakama ya Iringa wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari juu ya sakata  la Bangi ya kielelezo cha kesi kuibiwa katika mahakama hiyo. 

Baadhi ya Mahakimu na wanahabari wakiangalia Guba nje ya mahakama hiyo.

HATIMAYE lile sakata la mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, kukamatwa kwa tuhuma za kuiba bangi ambayo ni kidhibiti cha Mahakama,  limeingia katika sura mpya, baada ya Mahakama hiyo kulitaka jeshi la polisi kufanya upelelezi wa kina juu ya bangi hiyo walikoitoa.

Akizungumzia sakata hilo, la Mahakama yake kuhusika katika tukio la wizi wa bangi ambayo ni kidhibiti cha kesi,  kaimu msajili wa mahakama Wilaya ya Iringa Mhe. Godfrey Ntemi Isaya, amesema mahakama yake haijapotelewa na kidhibiti chochote, huku akilitaka jeshi la polisi mkoani Iringa kufanya kazi yake ya uchunguzi kwa umakini.

Mhe. Ntemi Isaya amesema bangi iliyokamatwa awali na kufikishwa mahakamani hapo iliteketezwa chini ya uangalizi wa jeshi hilo la Polisi, na kulitaka jeshi hilo kuonyesha bangi hiyo ilikoitoa, na siyo katika Mahakama hiyo.

Hata hivyo msajili huyo wa mahakama amesema hatua ya mtumishi wa  mahakama kuhusika na wizi huo ni suala binafsi, ila mahakama yake inalikanusha  jeshi hilo kusema Bangi imeibiwa katika Mahakama yake.

“Tunasikitika kuwa Polisi wametoa taarifa za kuibiwa kwa vielelezo vya mahakama katika vyombo vya habari kabla ya kuwasiliana na uongozi wa mahakama au mahakama husika ambayo ndiyo inatakiwa kuwa mlalamikaji, Katika taaarifa hii tunatambua wajibu mkubwa na umuhimu wa jeshi la polisi katika kukamata na kupeleka makosa ya jinai,” Alisema Mhe. Ntemi.

Aidha amesema wanakanusha kuwepo kwa upotevu wa kielelezo cha bangi  au kielelezo chochote kingine katika mhakama yake, kwani hata chumba cha kuhifadhia vidhibiti hakijavunjwa.

“Exhibit Room haijavunjwa, iko intact, tulikuwa na kielelezo Exh.P3 katika shauri  hilo la jinai Namba 24/2012 ambayo ilikuwa bangi Viroba 8, amri ya Mahakama ya kuteketeza ilitolewa tarehe 13/02/2013 na abangi hiyo iliteketezwa chini ya uangalizi wa ofisa wa jeshi la Polisi na kesi hiyo ilikwisha tarehe 13/2/2013 ambapo mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka miwili (2) gerezani,” alisema.

Pia mhe. Ntemi amesema kama ilivyo kesi nyingine za jinai, jeshi la polisi Iringa linatakiwa kufanya uchunguzi wa akina kuona bangi hiyo imepatikana wapi kwa kuwa haijatoka mahakamani kwake.

“Hatuna upotevu katika mazingira tatatizshi, Otherwise tungeripoti kituo cha Polisi, kwani stoo yetu ya vielelezo haijavunjwa na record ziko vizuri,” alifafanua.

Hata hivyo alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kutoa taarifa katika vyombo vya habari pasipo kufika katika mahakama hiyo na kuchunguza kile wanachokieleza.

“Hawajafika hapa kutuhoji sisi ambao ndiyo kwa kawaida andiyo waibiwa, wala hawajafanya mahojiano wala upekuzi katika Exhibit room yetu, kama mnavyoiona ipo salama kabisa, tunashauri jeshi la polisi liwe na utaratibu wa kufanya utafiti yakinifu kuhusu kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari,” Alisema.

Hatua hiyo imekuja baada ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kutoa taarifa za kumkamatwa kwa mlinzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kuiba bangi yenye uzito zaidi ya kg 300, ambayo ilikuwa ni kielelezo cha kesi katika Mahakama hiyo ya Wilaya na kumuuzia mwananchi Juma .

MWISHO

No comments:

Post a Comment