Sunday, June 30, 2013

KOMBE LA MUUNGANO LAFUNGULIWA- MBEYA CITY- :1 IGOWOLE - :0

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi- Mkoani Iringa Evarista Kalalu akipiga shuti kama ni ishara ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la Muungano.
 Uwanja wa shule ya msingi Igowole uliotumika katika ufunguzi huo wa Kombe la Muungano.
 Wachezaji wakiwa uwanjani kutimiza adhma yao.

 Mlinda mlango wa timu ya Mbeya City akijiweka tayari kuukabili mpira kutoka kwa wachezaji wa timu ya Igowole Sekondari.
 Mchezaji wa Igowole Sekondari akielekeza mashambulizi kwenye goli la timu ya Mbeya City.

 Wachezaji wa timu ya Mbeya City na Igowole (Jezi nyeupe kwa kijani) wakijiandaa kuupata mpira
 Mlinda mlango wa timu ya Mbeya City akiwa ulingoni.

HATIMAYE  mashindano ya kombe la Muungano yanayowashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo hufanyika kila mwaka kwa kuzishirikisha timu mbalimbali za mikoa ya kusini, yamefunguliwa rasmi huku katika kijiji cha Igowole wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Mashindano hayo ambayo ni ya 17 sasa tangu kuuanzishwa kwake, sasa yamelazimika kubadili taswira yake kwa kupanda kiwango cha washiriki, kutoka miaka 17 hadi kufikia miaka 20 na hiyo ni katika  msimu huu wa mwaka 2013.

Akizungumzia sababu za kuongeza umri wa washirikia mratibu  mkuu wa mashindano  hayo Daud Yasini alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya shiriki kughushi umri ili kukidhi vigezo vya usiriki katika michuano hiyo.

Yasini alisema katika mashindano hayo ya Kombe la Muungano kumekuwa na vijana wengi wakihitaji kushiriki na hivyo kulazimika kudanganya umri sahihi na sasa wameongeza kutoka miaka 17 ya sifa za mshiriki hadi kufikia miaka 20.

Yasini alisema jumla  ya timu 10 zitaweza kushiriki katika mashindano hayo  ambazo ni timu ya Mbeya City na Mbaspo Fc,kutoka mkoani Mbeya,  timu ya  Zamalek na Makambako united kutoka mkoani Njombe,  pamoja na timu ya  Holy familia kutoka mkoani Ruvuma, timu ambayo mwaka jana iliibuka mshindi wa mashindano hayo.

Yasini alisema katika mkoa wa  Iringa  kuna timu 4,  timu ya Rice fc na Ipogolo United  na timu ya Incoment  na Mucoba za  Mufindi.

Aidha alisema changamoto kubwa inayoikabili michuano hiyo kwa miaka yote iliyopita ilikuwa ni tatizo la umri ambapo  baadhi ya wachezaji kughushi umri, na sasa wameweza kukabiliana na hali hiyo ili kuwapa nafasi kubwa vijana walio wengi kushiriki michuano hiyo.

Akizungumzia zawadi za washindi kwa mawaka huu, Yasini alisema mashindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi Milioni tatu, ambapo mshindi wa pili atajinyakulia shilingi milioni moja na nusu , huku mwamuzi bora na mchezaji bora kila mmoja atapatiwa shilingi laki nne.

Hata hivyo mfungaji wa goli la kwanza la uzinduzi wa mashindano hayo aliweza kujichukulia shilingi elfu hamsini siku hiyo hiyo ya mashindano zawadi iliyoelekea upande wa timu ya Mbeya City ambayo iliibuka mshindi wa bao 1 bila dhidi ya Igowole Sekondari.

Bao hilo la Mbeya City ililiweza kuwekwa kimiani dakika ya 44 kipindi cha kwanza na mchezaji Frenk Hau mwenye jezi namba 10 huku Igowole wakikosa goli la penati lililopigwa na Gerlad Lubena wa Igowole Sekondari.

Hadi kipyenga kinapulizwa Mbeya City iliweza kuibuka mshindi wa bao 1:0 dhidi ya wapinzani wao  Igowole mechi iliyomalizika kwa amani huku umati mkubwa ukijitokeza kushuhudia mtanange huo na kuwa mashindano hayo yataendeshwa kwa muda wa mwezi mmoja.


MWISHO

No comments:

Post a Comment