Sunday, July 14, 2013

WATUMIA KONDOMU KAMA UREMBO



Picha ya Kondomu ya kike.
IMEFAHAMIKA kuwa kushindwa kupungua kwa ugonjwa hatari wa Ukimwi mkoani Iringa, kunatokana na baadhi ya wananchi kupotosha matumizi ya baadhi ya kinga za ugonjwa huo, huku Kondomu zikitumika kama mapambo, jambo linalokwamisha harakati za kuutokomeza ugonjwa huo.

Hayo yamezungumzwa na waratibu wa Ukimwi Wilayani Iringa, katika kikao cha wadau wa ukimwi kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Siasa ni Kilimo katika ofisi za Halmashaurio ya Wilaya hiyio ya Iringa.

Akifafanua juu ya changamoto hiyo mratibu ukimwi tiba, Dk. Duncan Ndimbo amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia Kondomu za kike kama mapambo ya masikio na wengine wakivaa kama Bangili.

Dr. Duncan Ndimbo amesema baadhi ya wasichana wamekuwa wakitumia Ringi ya juu ya kondomu kwa kuvaa masikioni kama hereni huku wengine wakivaa ringi hiyo mikononi kama bangili.

Amesema Kondomu za kike licha ya kuwa ni chache hizo ndizo zimekuwa hazitakiwi na hivyo kubadilishiwa matumizi yake, licha ya kuwa tatizo la ugonjwa wa ukimwi bado ni tatizo kubwa.

Naye mratibu wa ukimwi Wilaya ya Iringa Odia Hezroni amesema waathirika wengi baada ya kutumia dawa za kuongeza siku huacha na baada ya kufa kwa kukatisha dozi ndugu zao huamini kuwa wamerogwa, huku pombe ya Ulanzi ikionekana kuwa ni chanzo cha uwepo wa ngono zembe zinazochangia uwepo wa maambukizi ya ugonjwa swa ukimwi.


Aidha Odia amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inakabiliwa na tatizo la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa asilimia 9.1 na tatizo kubwa ni tabia za kurithi wajane, pamoja na Ulevi uliokithiri wa Pombe aina ya Ulanzi
.

No comments:

Post a Comment