Meneja mkuu wa benki ya wananchi Mufindi (MuCoBa) akisoma taarifa za kibenki katika mkutano wa 14.
Maofisa kutoka benki kuu Tanzania BoT - wakiwa katika mkutano huo wa benki ya MuCoBa Wilayani Mufindi Iringa.
Ofisa mikopo wa benki ya MuCoBa Benny Mahenge akitoa ufafanuzi wa masuala ya mikopo katika mkutano huo.
ZAIDI ya shilingi Bilioni 8.8 zimetolewa na benki ya Mufindi
Community Bank (MuCoBa) na kukopeshwa kwa wananchi zaidi ya elfu 5 Mkoani
Iringa kwa lengo la kukuza mitaji yao na kuboresha maisha katika kipindi cha
mwaka 2012.
Hayo yalizungumzwa na meneja mkuu wa MuCoBa Danny Mpogole wakati
akitoa taarifa za maendeleo ya benki hiyo katika mkutano wa 14 wa wanahisa wa
mwaka 2013 katika ukumbi wa Sourthen Hingland katika mji wa Mafinga mkoani
Iringa.
Mpogole alisema mikopo hiyo ni ongezeko la asilimia 1.7 kwa
mwaka 2012 kutoka asilimia 1.4 ya mwaka 2012 huku mapato ya mikopo hiyo
yakichangia asilimia 81.2 ya mapato yote ya benki ya MuCoBa.
Aidha alisema changamoto kubwa ya benki hiyo ni urejeshaji hafifu
wa huku baadhi ya wateja wakiwa si waaminifu kwa kushindwa kulipa madeni ya
mikopo yao na hivyo malengo ya benki kusuasua.
Alisema MuCoBa imefanikiwa kupata faida ya shilingi Milioni
240.2 na hivyo kukaribia malengo ya faida ya shilingi Milioni 240.3 huku
mtaji ukikua kutoa 443 mwaka 2011 hadi kufia Milioni 593.5 kwa mwaka 2012.
“Pamoja na changamoto zilizokuwepo mwaka 2012, benki
ilifanikiwa kupata faida ya shilingi Milioni 240.2 ikilinganishwa na lengo la
sh. 240.3, huku mwaka 2011 faida ilikuwa sh. Mil;ioni 227.9,” Alisema Mpogole.
Alisema faida ya benki hiyo imeathiriwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya wateja kutokuwa waaminifu katika kurejesha madeni ya mikopo yao, na
hiyo inatokana na kuyumba kwa biashara ya mbao hasa kutokana na wafanyabiashara
walio wengi kuwa ndiyo wateja wa benki hiyo.
Mpogole alisema changamoto hizo pia zimesababisha kupungua kwa
mapato yatokanayo na mikopo kwa sababu ya mikopo Chechefu isiyolipika vizuri na
kufuata muda uliopangwa.
Alisema benki inaendelea kuweka vipaumbele katika utoaji wa huduma kwa wateja wadogo wadogo na wale wa kati na hivyo kupanua mtandao wake kwa kutoa huduma zake kupitia Saccos na vikundi mbalimbali.
Alisema pia benki ya MuCoBa inaendelea kupanua huduma zake kwa wafanyakazi katika taasisi za Umma na za binafsi ili kutoa huduma kwa jamii nzima na kuwa matarajio ya benki kwa mwaka 2013 ni kuboresha zaidi huduma zake.
"Tutahakikisha mwaka 2013 tunaboresha huduma za benki ikiwa pamoja na kuwafikia zaidi wananchi wa vijijini, kwani tayari tumemaliza ofisi yetu ya Igowole na sasa ofisi hiyo ipo tayari na imeanza kutumika kwa kutoa huduma za kibenki," Alisema.
Aidha Mpogole alisema tayari benki imeanzisha huduma ya mashine maalumu za kutolea fedha (ATM) kwa lengo la kupunguza msongamano ndani ya benki na kuwawezesha wateja kupata fedha katika muda muafaka wakati wsowote katika maeneo mengine nje ya Mafinga.
Kaimu mwenyekiti wa MuCoBa Ernest Usangira alisema katika
kukabiliana na changamoto ya mikopo chechefu benki imeanza
kufuatilia madeni kwa wakopaji huku wakijidhatiti kuimarisha vyanzo mbalimbali
vya fedha kama akiba na mikopo kutoka katika taasisi nyingine za kifedha ili kuwa
na fedha za kutosha kwa ajili ya kukopesha na hivyo kuongeza mapato ya benki.
Benny Mahenge ofisa mikopo wa MuCoBa alisema katika jitihada za
kukabiliana na hali hiyo wanahisa waliongezea mtaji wa shilingi Milioni 593.5
mwaka 2012 na hivyo benki kufanya ongezeko la asilimia 25.
Mahenge alisema kwa taarifa za benki kuu (BoT) zinaonyesha benki
hiyo ina mtaji wa shilingi Milioni 921, mtaji ambao upo chini ya vigezo vya
sifa za benki za wananchi, kwani BoT inazitaka benki hizo za wananchi kuwa na
mtaji wa shilingi Bilioni 2.
MWISHO
No comments:
Post a Comment