Hamis Lupenja afisa mwandamizi elimu TRA jijini Dar es salaam akitoa elimu kwa wafanyabiashara mjini Iringa.
Kyalo Masavi fundi mkuu wa kampuni ya Bolsto kampuni ya kutengeneza mashine za kutolea lisiti akiwa na Soga Pius katika mkutano baina ya wafanyabiashara na maofisa wa TRA mkoa wa Iringa.
Gerlad Hilly- afisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa malipo ya kodi TRA Mkoa wa Iringa
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda (TCCRA) mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu, akiwahimiza wafanyabiashara kujiunga na chemba hiyo ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wafanyabiashara wakisikiliza kwa makini mafunzo juu ya matumizi ya mashine za kutolea lisiti, katika mafunzo ya siku moja mjini Iringa.
Meneja wa kituo cha Radio Country fm (wa pili kulia) Huruma Mgaya akiwa katika mafunzo hayo ya wafanyabiashara.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwasikiliza maofisa wa TRA katika mafunzo hayo (aliyeshika kidevu) ni Ditto Kalole mfanyabiashara wa Miyomboni mjini Iringa.
Ditto Kalole na kaka yake Jackson Kalole (mwenye koti jeusi ndani T.shirt nyeupe)wakisikiliza mafunzo hayo.
Kaimu meneja wa TRA mkoa wa Iringa Swalehe Byarugaba akitoa elimu kwa wafanyabiashara(Hawapo pichani).
Wakiangalia mashine za "Bolsto" zilizoingia mkataba na TRA nchini.
Mashine za kutolea lisiti zinazotengenezwa na kampuni ya Bolsto, kampuni ambayo imetangazwa na TRA kuwa ni kati ya makampuni bora yenye vifaa imara.
Wakionyeshana baadhi ya mashine, huku nyingine zikiwa hazitumii nishati ya umeme, na katika muundo (Size) tofauti, ndogo, zakati na hata ndogo kabisa kwa namna mteja anavyohitaji.
Bango la Kampuni ya mashine za Bolsto- lililopelekwa katika ukumbi wa mafunzo ya wafanyabiashara.
Mashine za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni ya Bolsto Solution Limited.
HATIMAYE wafanyabiashara wa Kariakoo jijini
Dar es Salaam, ambao wamekuwa hawatoi risiti zenye maelezo sahihi kwa wafanyabiashara wa mikoani, wameanza kubanwa baada ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuanza ukaguzi wa vielelezo zikiwemo mashine za kutolea risiti.
Hayo yamezungumzwa na ofisa
mwandamizi wa elimu TRA nchini Hamis Lupenja
wakati akitoa mafunzo kwa
wafanyabiashara mkoani Iringa, wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwalalamikia hatua hiyo ya wafanyabiashara
hao wa Kariakoo, mafunzo yaliyoandaliwa na TRA na kufanyika katika Hotel ya Kalenga mjini Iringa.
Lupenja amesema ili kuhakikisha
wafanyabiashara wa mikoani hawazurumiwi haki za kibiashara watawabana
wafanyabiashara wa Kariakoo ambao wamekuwa wakiendesha shughuli zao kiujanja
ujanja kwa lengo la kuiibia serikali.
Aidha Lupenja amesema katika
kuhakikisha dhuruma hiyo inakomeshwa tayari TRA imeingia mkataba na makampuni
11 ya utengenezaji wa mashine za kutolea risiti, ili kutekeleza sheria ya kodi
ya ongezeko la thamani kifungu namba 148.
Pia amesema TRA imeingia mkataba na wasambazaji wa
mashine thabiti za kutolea lisiti, wakiwemo Bolsto Solutions Limited wa jijini
Dar es salaam ili kuwaepusha wafanyabiashara kutoingia hasara ya kununua
mashine zisizofaa.
Kyalo Masavi mratibu wa ufundi wa
kampuni ya Bolsto Solution Limited amesema ili kuwainua wafanyabiashara nchini,
Bolsto imeboresha vifaa hivyo vya kutolea lisiti kwa kutoa muda wa ziada (Guarantee)
ya miaka mitatu pamoja na matengenezo ya mashine hizo yakitolewa bila gharama
zozote.
“Kampuni yetu ya Bolsto imekusudia
kuwasaidia wafanyabiashara, kwanza mashine zetu tunauza kwa gharama ndogo,
tunatoa Guarantee ya miaka mitatu na pia tunao mafundi wakliobobea katika
utaalamu wa vifaa hivyo, lengo kuu ni kutowaingiza katika hasara lwafanyabiashara,”
alisema Masavi.
Hatua ya TRA kuingia mkataba na
kampuni hizo ikiwemo ya Bolsto inatokana na awali wafanyabiashara kulalamikia uwepo
wa baadhi ya mashine kuwa mbovu na hivyo wafanyabiashara kupata hasara kubwa.
Jackson Kalole mfanyabiashara mjini Iringa, amesema kuna haja kwa TRA kuwabana wauzaji wa mashine feki kwa kuwa nyingi zimeharibika na kuwasababishia hasara, ikiwa pamoja na kukabiliana na tatizo la maofisa Vishoka wa Mamlaka hiyo ambao wamekuwa wakiwasumbua kwa manufaa yao binafsi.
"Mnatusaidiaje sisi wafanyabiashara kuhusiana na maofisa Vishoka wanaojifanya wametoka TRA, kwani hao ni kikwazo kwetu, na pia tayari mmewakamata vishoka hao wangapi??" Alisema Kalole.
Akitoa ufafanuzi wa tatizo la vishoka kaimu meneja wa TRA mkoa wa
Iringa Swalehe Byarugaba amesema wafanyabiashara wanatakiwa kutoa taarifa TRA haraka pindi wanaposhitukia uwepo wa watu hao katika maduka yao.
"Kuna zile namba za bure, ukiona kuna afisa unamtilia shaka, tujulishe kwa kutupigia simu, au mwambie akupe kitambulisho chake cha kazi, na katika simu tutabaini kama ofisa huyo ni halali au laa, au hata kama ni ofisa wa TRA kama amepangiwa katika eneo hilo kufanya oparesheni," Alisema Byarugaba.
Pia amewataka wafanyabiashara kutokuwa waoga katika
kuzitumia mashine hizo za kutolea lisiti, huku akiwataka wasiwaogope maofisa wa
TRA, na kama kuna changamoto zozote baina yao na maofisa hao wafike katika
ofisi za TRA ili kujadiliana kwa pamoja.
“Niwaombeni ndugu zangu, msituogope
sisi maofisa wa TRA, hakuna uadui baina yetu, tunatakiwa kufanya kazi kwa
ushirikiano lengo letu ni moja kukuza pato la Taifa letu, na kama kuna ofisa
yeyote unamtilia shaka katika zoezi la ukusanyaji wa kodi ninaomba tuwasiliane
au mfike katika ofisi zetu za TRA mkoa,” Alisema Byarugaba.
No comments:
Post a Comment