Bango la uzinduzi wa Maktaba ya shule ya sekondari JJ. Mungai, iliyopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Bw. Bernad Makali akiwa tayari amezindua maktaba ya JJ. Mungai.Kibao cha uzinduzi wa jengo la Maktaba, ambacho kinaweka kumbukumbu ya wafadhiri hao kusaidia ujenzi wa Mktaba hiyo ya kisasa ya JJ. Mungai.
Baadhi tu ya Vitabu vilivyopo katika maktaba hiyo mpya ya kisasa, iliyojengwa kwa udhamini wa asas ya kiraia ya nchini Itali ya CIC.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bw. Mariano Mwanyigu akiwa na serikali ya wanafunzi wa shule hiyo ya JJ. Mungai Amanda Ukwembe rais wa serikali ya wanafunzi wa JJ. Mungai akiwa na Winfrida Masanja ambaye ni katibu wa serikali ya wanafunzi wa shule ya JJ. Mungai.
Wanafunzi wa JJ. Mungai wakiwa katika hafla hiyo, ndani ya ukumbi wa shule.
Wanafunzi wa JJ. Mungai wa kidato cha tatu na nne wakiwa katika hafla hiyo.
Bi. Anitha Masaki ambaye ni afisa mradi wa Form for Women Educationist (FAWE) mradi unaowafadhili wanafunzi zaidi ya 40 wa sekondari ya JJ. Mungai . Huku FAWE wakiwa ndiyo waliowatafuta CIC waliojenga Maktaba hiyo.
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Baadhi ya walimu wakiwa katika hafla hiyo.
Ofisa elimu taaluma mkoa wa Iringa Auzebio Mtavangu (Katikati mwenye Tai) akiwa na baadhi ya viongozi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa.
Bi. Asnati Ndelwa mmoja wa wasichana waliofanikiwa kielimu kupitia mradi wa FAWE, akitoa ushuhuda wa FAWE kumuokoa katika umasikini ambao ungesababisha akose elimu.
Bi. Neema Kitundu Mratibu wa mradi wa FAWE akitoa taarifa za shughuli wanazofanya FAWE Taifa kwa wanafunzi wa kike wasio na uwezo.
Bi. Barbara Bianchi Bonomi rais wa asas ya kiitalianao ya CIC akitoa taarifa ya mradi wake katika hafla hiyo.
Bi. Silvana Lauria mshauri wa rais wa mradi wa CIC akitoa ufafanuzi wa namna ya kuwasaidia wanafunzi wa JJ. Mungai
Baadhi ya anafunzi wa JJ. Mungai wakisikiliza maelezo kutoka kwa ugeni wa hafla hiyo ya uziinduzi wa maktaba ya Kisasa.
Mwanafunzi Edna Kapugi (Aliyeshika Kipaza sauti "Mic") akisoma Lisara ya wanafunzi wa JJ. Mungai katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Maktaba ya kisasa, akiwa na Nancy Chalamila.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo Bw. Bernad Makali akisoma risala ya uzinduzi wa maktaba.
Mkuu wa shule ya sekondari JJ. Mungai Mwalimu Mariano Mwanyigu, akitoa taarifa ya shule yake katika hafla hiyo.
Jengo la maktaba ambalo limezinduliwa kwa ajili ya kutoa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na wananchi wanaopenda kusoma vitabu.
Bango la uzinduzi.
Ndani ya maktaba hiyo ya kisasa vitabu tayari vinapatikana.
SHULE ya sekondari JJ. Mungai imefanikiwa kujenga Maktaba iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 132, kwa lengo la kutoa fulsa kwa wanafunzi kujisomea ili kuongeza uelewa zaidi.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo mkuu wa shule ya sekondari JJ. Mungai, mwalimu Mariano Mwanyigu amesema ujenzi huo ni ufadhili wa wafadhili kutoka nchi ya Itali kupitia asas ya Chidren In Crisis (CIC).
Mwalimu Mwanyigu amesema wafadhili hao wametokana na juhudi za mradi wa Forum for Africa Women Educations (FAWE) kutokana na mradi huo kutambua hitaji la wanafunzi wa shule yake.
Aidha Mwanyigu amesema mradi wa FAWE umekuwa ukitoa misaada mbalimbali, kwa wanafunzi wa kike 40 wanaotoka katika mazingira magumu na wanafunzi yatima, na kuwa FAWE hutoa huduma ya mahitaji mbalimbali ya wanafunzi shuleni hapo, ikiwemo kuwalipia ada, kuwanunulia Sare za shule, hutoa Magodolo kwa wanafunzi wa Bweni, nauli kwa wanafunzi wa kutwa pamoja na vifaa vya kujifunzia.
Mkuu huyo wa shule amesema wafadhili hao wa Kiitaliano CIC wamechangia zaidi ya shilingi Milioni 110, huku shule yake ikichangia zaidi ya shilingi Milioni 21.8.
Hata hivyo Mwanyigu amesema licha ya kujenga maktaba hiyo pia wamefanikiwa kujenga Bweni la wavulana, huku changamoto mbalimbali bado zikiwa zinaikabili shule yake, kama vitabu kutotoshereza mahitaji ya walengwa, uchache wa Samani pamoja na kutokuwepo Mkutubi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya huduma za Maktaba.
MWISHO
No comments:
Post a Comment