Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akisoma hotuba katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi cha Donbosco kilichopo mjini Iringa.
Mkuu wa Chuo cha ufundi Donbosco, Padre Abery Njeru (wa kwanza kushoto) akiwa katika ukumbi huo, kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr. Christine Ishengoma akiteta jambo na mkurugenzi wa vyuo vya ufundi kanda ya kusini, Bi. Monica Mbelle.
Mmoja wa wakuu wa vyuo vya ufundi akipokea msaada wa Komyuta kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma, vifaa vyenye lengo la kuongeza ujuzi katika vyuo vya VETA.
Akipokea msaada wa Kompyuta.
Mwalimu wa chuo cha ufundi Donbosco, akiongoza kwaya ya chuo hicho katika kutoa ujumbe katika mkutano huo wa wakuu wa vyuo vya VETA nyanda za juu kusini.
washiriki wa mkutano huo wakiwa ndani ya ukumbi wa chuo cha ufundi Donbosco mjini Iringa.
Mratibu wa vyuo vya mafunzo ya ufundi nyanda VETA - za juu kusini Bw. John Mwanja akitoa taarifa kwa washiriki wa mafunzo hayo katika chuo cha ufundi cha Donbosco mjini Iringa
Mkurugenzi wa VETA nyanda za kusini Bi. Monica Mbelle akitoa taarifa ya vyuo hivyo na namna ya uendeshaji wa majukumu yake, mbele ya wakuu wa vyuo hivyo kutoka mkoa wa Njombe, Iringa, Ruvuma na mkoa wa Rukwa.
Mwenyekiti wa bodi ya wakuu wa vyuo vikuu nyanda ya kusini Bw. Kabaka Ndenda akizungumza katika mkutano huo wa siku mbili wa wakuu wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi (VETA).
Wakuu wa vyuo vya VETA wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa chuo cha ufundi DONBOSCO mjini Iringa
Washiriki mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja.
WITO umetolewa kwa wasomi wa vyuo vikuu kote nchini, kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi "Veta", ili kujiongezea ujuzi na maarifa ya kufanya kazi, kwa lengo la kujiajiri wenyewe katika sekta binafsi, hatua ambayo itapunguza utegemezi wa ajira serikalini.
RAI hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma, wakati akifungua mkutano wa wakuu wa vyuo vya VETA, mkutano wenye lengo la kupeana mikakati juu ya utaratibu wa uendeshaji wa vyuo katika mfumo mpya wa Compitance Base Assesment (CBI) - mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Donbosco, kilichopo Manispaa ya mji wa Iringa.
Dr. Ishengoma amesema pia wazazi na walezi wanapaswa kuachana na dhana potofu ya kuwa vyuo vya Veta vipo kwa ajili ya wasio na elimu pekee, huku akiitaka kuwapeleka vijana wao katika vyuo hivyo vya ufundi vilivyosajiliwa, na kuwataka wakuu wa vyuo kuajiri walimu wenye sifa.
"Mimi ninawaomba vijana hawa wanaomaliza vyuo vikuu nao waongezee ujuzi, wajiunge katika vyuo vyetu vya vyeta, ili waweze kupata mafunzo kwa vitendo, na pia niiombe jamii iondokane na mawazo potofu, wananchi lazima tubadilike na kuachana na mawazo haya, ya kusema wanaosema Veta hawana elimu, wajue ufundi stadi ni muhimu sana kwa maendeleo yetu, wajifunze kwa muda mfupi Veta ni mkombozi wa ajira," Alisema.
Mkurugenzi wa vyuo vya Veta Nyanda za juu kusini Monica Mbelle amesema Kanda ya kusini ina jumla ya vyuo vya veta 74, huku mkoa wa Iringa ukiwa na vyuo 29, mkoa wa Njombe vyuo 23 Ruvuma pamoja na mkoa wa Ruvuma 22.
Bi. Mbelle amesema katika msimu wa mwaka 2013/ 14 Veta inampango wa kujenga vyuo vya Veta katika wilaya ya Ludewa, Chuo cha Wilaya ya Namtumbo pamoja na ujenzi wa chuo cha Mkoa wa Njombe.
Aidha Mbelle alisema vyuo vya VETA vinatoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuongeza tija na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wananchi.
"Katika vyuo vyetu tunatoa mafunzo ya muda mfupi ya wiki moja hadi miezi sita, na muda mrefu mwaka miwili hadi miaka mitatu, na mafunzo haya yanatolewa kwa sekta rasmi na sekta isiyo rasmi, hii inawasaidia wananchi kupata stadi za kazi ili waweze kuongeza tija za uzalishaji na ubora wa bidhaa," Alisema Mbelle.
Naye Bw. Kabaka Ndenda Mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya ufundi kanda ya kusini alisema wananchi wanatakiwa kuvitumia vyuo hivyo katika kutafuta maendeleo, huku akiitaka serikali kuwasaidia vijana kwa kutumia nguvu kutangaza bidhaa zinazozalishwa na vijana wa vyuo vya Ufundi VETA.
MWISHO
No comments:
Post a Comment