Mkuu wa Wilaya ya Iringa Vijijini Dr. Retisia Warioba, akikabidhi Mwenge kwa mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw. Gerlady Guninita, katika eneo la Uhambingeto.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw. Gerlady Guninita akipokea Mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa Wilaya ya Kilolo Dr. Retisia Warioba, makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Uhambingeto Kilolo mkoani Iringa.
"Ninaupokea Mwenge huu wa Uhuru, nitahakikisha ninautunza na kuulinda, mpaka nitakapoukabithi kwa Wilaya ya Iringa Mjini hapo kesho, Ee Mwenyezi Mungu unisaidie," Akisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilolo, kama ni ishara ya kuheshimu alama hiyo ya Uhuru wa Tanzania.
Baadhi ya viongoziwa Wilaya ya Kilolo wakiushika Mwenge kama ishara ya kuupokea Mwenge wa uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali, ikiwa pamoja na kuzindua miradi mbalimbali na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya maendeleo.
Profesa Peter Msolla, ambaye ni mbunge wa jimbo la Wilaya ya Kilolo akipokea Mwenge wa Uhuru, katika shule ya Sekondari Uhambingeto Kilolo.
Wanafunzi wa shule ya sekindari Uhambingeto wakiupokea mwenge, ambao pamoja na mambo mengine ulizindua Clab ya wanafunzi ya kupinga na kupambana na Rushwa.
Bango la uzinduzi wa majengo ya shule ya sekondari Uhambingeto.
Baadhi ya nyumba za walimu katika shule ya sekondari Uhambingeto, ambayo yamezinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Nyumba ya walimu (Two in One) katika shule ya Sekondari Uhambingeto.
Wananchi wa kijiji cha Vitono- Kilolo wakiwa wameepukana na adha ya maji, ambayo walikuwa wakiipata umbali wa km 20, mradi huo umezinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Vitono (mwenye Tshirt ya kijani) akitoa shukrani zake kwa kupata huduma ya maji ambayo walikuwa wakiipata umbali mrefu, kulia ni mbunge Profesa Peter Msolla.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw. Juma Ali Simai(katikati) akitoa usia kwa wananchi juu ya kuutunza mradi huo wa maji katika kijiji cha Vitono-Kilolo.
Jengo la Zahanati ya ya kijiji cha Kipaduka - kilolo ambao ni moja ya miradi iliyozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru, ujenzi uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 30.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya jengo la Zahanati katika kijiji cha Kipaduka- Kilolo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kipaduka wakishuhudia uzinduzi wa Zahanati yao.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika shule ya sekondari "Lord's Hill" iliyopo Ilula katika Wilaya ya Kilolo, moja ya miradi ambayo imezinduliwa na Mwenge huo.
Raia wa kigeni wakishangiria Mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua shule ya sekondari Lord's Hill.
Mkuu wa shule ya sekondari Lord's Hill Bw. Jeremia Kiswaga naye akionyesha uzalendo wake kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru, mara baada ya kuzindua rasmi shule yake.
ZAIDI ya shilingi Bilioni 1.38 zimetumika katika ujenzi wa miradi 6 ya huduma za jamii katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, lengo likiwa ni kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabiri wananchi.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, mbele ya viongozi wa
mbio za mwenge kitaifa, kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bw. Benson Kilangi amesema miradi ambao imekamilika kwa kutumia fedha hiyo ni mradi wa maji wa Vitono, uliotumia zaidi ya shilingi Milioni 352 huku mradi wa ujenzi wa
barabara ya Ruahambuyuni - Msosa ukigharimu zaidi ya shilingi Milioni 109.87 huku mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kipaduka ukigharimu zaidi ya shilingi Milioni 30.
Bw. Kilangi amesema kukamilika kwa ujenzi wa miradi hiyo kutasaidia kuleta ufanisi wa maendeleo kwa wananchi, kwa kupata huduma hizo jirani nakwa urahisi tofauti na awali.
Naye Luten Speratus Lubinga kiongozi namba mbili wa mbio za mwenge Kitaifa amesema fedha hizo zitaleta tija na kutoa huduma bora kwa jamii, kwa kupunguza changamoto za mahitaji ya huduma muhimu.
Hata hivyo Kiongozi namba moja wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Ali Simai amewataka wananchi kuitunza na kuithamini miradi hiyo ili iwasaidie kwa kipindi kirefu.
Mwenge wa Uhuru upo mkoani Iringa ambapo unataraji kufikia kilele chake kesho tarehe 14, kwa kuzimwa mkoani hapa, ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa wanataraji kuhudhuria sherehe hiyo, yakiwemo maadhimisho ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
MWISHO
No comments:
Post a Comment