Friday, October 11, 2013

MWENGE WAWAPAGAWISHA WILAYA YA IRINGA

ZIKIWA zimebaki siku chache tu ili Mwenge wa Uhuru uzimwe baada ya kukimbizwa mikoa yote ya Tanzania, kwa kuvipitia vijiji, Kata na Wilaya za mikoa yote, sasa mwenge huo upo mkoani Iringa mabapo utazimwa tarehe 14 mwezi huu wa kumi katika siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa muasisi wa nchi yetu Mwalimu Jurius Kambarage Nyerere, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa nayo imezindua Miradi 11 ya maendeleo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Ali Simai akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Iringa wakati wa makabidhiano ya Mwenge baina ya Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Iringa.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda na sekondari ya Ufundi Ifunda katika Wilaya ya Iringa, wakishuhudia uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha eneo hilo la Ifunda.
 Mwenge ukikimbizwa katika moja ya maeneo ya Ifunda Wilayani Iringa, lengo kuu likiwa ni kuchochea maendeleo kwa kuzindua miradi mbalimbali.
 Viongozi wa Mbio za mwenge kitaifa, pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Iringa wakiwa katika  mradi wa vitaru vya miche ya miti katika shule ya msingi Lyandembela.
 Jiwe la msingi la mradi wa Bwawa la ufugaji wa Samaki katika Kata ya Mgama Wilayani Kilolo, mradi ambao utaongeza kipato kwa jamii pindi tu utakapokamilika.
 Bw. Jimmy Chandafa ofisa mtendaji wa kijiji cha Mgama akisoma taarifa ya ukarabati  wa mradi wa barabara ya Mgama-Wenda, zilizopo Wilaya ya Iringa.
 Wananchi wa kijiji cha Lyamgungwe wakishangilia ujio wa Mwenge ambao umeweza kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
 Bw. Juma Ali Simai kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2013 akizindua mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Lyamgungwe kilichopo Wilaya ya Iringa.
 "Ahaa kumbe yanatoka" Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Bw. Juma Ali Simai akifungua maji ya bomba mara tu baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa maji ya bomba katika kijiji cha Lyamgungwe Wilayani Iringa.
 "Haya jitwishe maji haya, hamtapata shida tena ya kufuata mbali huduma hii ya maji," Ni maneno ya kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa Bw. Juma Ali Simai baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Lyamgungwe Wilayani Iringa.
 Shule ya msingi Igunda ambayo imezinduliwa na mbio za mwenge, ambapo kukamilika kwa ujenzi wa shule hii kutapunguza umbali wa wanafunzi wa kijiji cha Igunda ambao walikuwa wakitembea zaidi ya km 5 kufuata elimu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kalenga, iliyopo Wilaya ya Iringa wakiwa katika majaribio ya Somo la Sayansi baada ya shule yao kufunguliwa jengo la Maabara itakayowawezesha kuendesha elimu hiyo ya Sayansi kwa vitendo, Maabara iliyozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru. 
 Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakicheza kushangilia Mwenge wa Uhuru.  
 Wanafunzi wa shule ya sekondari Kalenga wakiwa katika jengo la Maabara, baada ya kuzinduliwa rasmi na mbio za mWenge wa Uhuru.
 Mwanafunzi Herena Msofu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kalenga Wilaya ya Iringa, akitoa maelezo ya juu ya matumizi ya vifaa vya kisayansi vilivyopo katika maabara hiyo ambayo imezinduliwa rasmi na mbio za Mwenge wa Uhuru.
 Wananchi wa eneo la Nzihi katika Wilaya ya Iringa eneo ambalo Mwenge wa Uhuru umelala hapo ili kukamirisha uzinduzi wa miradi katika Wilaya hiyo mkoani Iringa.
 "Huku juu ndiyo poa, tunaona vizuri bila shida," Ni kama wamesema wananchi hao wa kijiji cha Nzihi ambao walilazimika kupanda juu ya miti ili kuuona vyema Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuingia katika kijiji hicho.
 
Watumishi na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Wakicheza Kwaito kushangiria ujio wa mwenge wa uhuru katika Wilaya yao.

No comments:

Post a Comment