Saturday, November 2, 2013

MADEREVA WA BODABODA WAPATIWA ELIMU NA PIKIPIKI BURE KUDUMISHA DORIA

 Mwenyekiti wa chama cha waendesha Bodaboda mjini Iringa Bw. Joseph Mwambobe akijaribu moja ya Usafiri wa Pikipiki alioupokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabara Bw. Salim Abri Asas, katika hafla ya kukabidhiwa vyeti madereva 100 waliohitimu mafunzo ya udereva huo..
 Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa Pikipiki, wakiapa juu ya kutii sheria bila shuruti,  mafunzo yaliyodhaminiwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri Asas-
 "Kiapo" Sisi madereva wa pikipiki, tunaapa ya kuwa.....


 "Nitahakikisha ninakuwa mwangalifu kwa kufuata sheria, na mara tu ninapopanda Pikipiki mimi na abiria wangu tunavaa kofia ngumu,"  Ni kati ya maneno ya kiapo cha madereva hao wa Pikipiki.
 Bw. Salim- akipeana mkono nammoja wa wahitimu wa mafunzo ya udereva wa pikipiki, ambapo pia wahitimu hao walipatiwa vyeti vya mafunzo hayo.
 Kulia ni RTO  SP Panfil Honono akiwa katika hafla hiyo ya madereva 100 kupatiwa vyeti vya uhitimu wa mafunzo hayo yaliyoambatana na msaada wa pikipiki mbili zilizotolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri Asas, ili zisaidie kufanya dolia ya kudumisha usalama wa barabarani.
 Muhitimu akipokea cheti chake cha kuhitimu elimu ya udereva wa Pikipiki, mafunzo yaliyotolewa kwa Udhamini wa Bw. Salim Abri Asas, ambapo aliwalipia ada madereva hao 100.

 "Hongera sana"  Ni maneno ya mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani wakati akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.


 Muhitimu wa mafunzo ya udereva wa Pikipiki akipeana mkono na mkaguzi wa vyombo vya moto barabarani (Vehicle Inspector) wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa afande Steve,  ambaye pia ni mwalimu wa Vipindi vya  usalama wa barabarani, kupitia vyombo vya habari. km Radio..
 Mmoja wa wahitimu wa udereva wa bodaboda akipeana mkono na RTO SP Honono katika hafla ya kupatiwa vyeti vya uhitimu wa mafunzo ya udereva wa Pikipiki.

Mmoja wawahitimu wa elimu  ya Udereva wa Bodaboda, akipokea cheti.
 Madereva wa Pikipiki wakiwa  nje ya ukumbi wa Hallfear, uliopo Kata ya Miyomboni / Kitanzini mjini Iringa, mara baada ya kumaliza shughuli ya kutunukiwa vyeti vya uhitimu wa mafunzo hayo ya udereva wa Bodaboda.

 Cheti cha uhitimu wa mafunzo wa udereva wa Pikipiki.

<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>.
WAHITIMU wa mafunzo ya udereva mkoani Iringa, wamepatiwa Pikipiki za bure kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi usalama barabarani na kwa kundi hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa kutofuata sheria za usalama wa barabara na hivyo kusababisha ongezeko la ajari.

Akikabidhi msaada wa Pikipiki mbili katika ukumbi wa Hallfear kwa uongozi wa chama cha waendesha Bodaboda mjini Iringa, mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama mkoani Iringa Bw. Salim Abri “Asas” amesema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi yake kwa chama hicho cha waendesha Bodaboda, pekipiki ambazo zitatumika katika dolia.

Bw. Salim amesema msaada huo ni katika kutambua umuhimu  kazi hiyo ya udereva wa Pikipiki ambao kwa kiwango kikubwa umetoa ajira kwa kundi kubwa la vijana nchini.

Salim amesema kamati yake ya ulinzi na usalama barabara itahakikisha ajira hiyo inakuwa salama kwa kutoa elimu kwa madereva wa pikipiki kwa lengo la kupunguza ajali na vifo vitokanavyo na usafiri huo.

Aidha wahitimu hao 100 wa mafunzo ya udereva wamelipiwa ada ya elimu hiyo ya udereva huku mwenyekiti huyo akitoa nafasi nyingine kwa madereva 100 ambapo pia wartapatiwa elimu hiyo.

Hata hivyo Bw. Salimu ameahidi kuongeza msaada wa Pikipiki nyingine mbili ili kuifanya kazi hiyo ya dolia kwa uhakika na kufanikisha mpango wa kutokomeza ajali na vifo vitokanavyo na usafiri huo wa pikipiki., huku akiwataka madereva hao kutobweteka kwa kuishia kazi hiyo ya udereva wa Pikipiki bali kufanya jitihada za kusonga mbele.

“Sidhani kama kazi hii ya udereva wa Pikipiki mtafanya hata muwapo wazee, cha msingi mnachopaswa kukifanya ni kuwa na mawazo ya kusonga mbele muwe madereva wa magari, msiishie hapa kwenye kazi hii ya bodaboda tu!! Lakini ipo haja ya kuanzisha Saccos yenu ili muweze kukopeshana fedha na kuweza kumiliki Pikipiki zenu, maana ninaambiwa kuwa hapa baadhi yenu Pikipiki hizi siyo zenu,” Alisema Salim.


Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani kupitia jeshi la Polisi (OCD)  SP Panfil Honono amewataka madereva hao kuwa na nidhamu katika kazi hiyo na kusimamia sheria za barabarani bila shuruti ili ajira hiyo iwe na thamani katika jamii.

Naye mwakirishi wa Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa SP Zakaria Benard amewataka madereva hao kujihami katika kazi hiyo, kwa kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa ikiwa pamoja na kuacha tamaa ya kuwachukua abiria wanaowatilia shaka.

“Mtu kama humfahamu siyo lazima umpeleke anakotaka, lakini pia muwe makini kwa kuwatambua wateja wenu, muulize jina huku ukimuhoji baadhi ya maswali, ambavyo yatakuwa ni msaada kwako, kitu kingine ndugu zangu!! Acheni tamaa, mfano unakuta mteja humfahamu anakukodi umpeleke kituo kimoja, unafikanae katika kituo kile alichosema nataka kufika, anasema umpeleke mbele zaidi, hapo utambue kuwa huyo siyo abiria mwema, kataa na kisha muache hapo na urudi katika kituo chako, tunafahamu kumekuwa na wimbi la utekaji na hata mauaji mnafanyiwa kwa kutumia njia hizo za kuwakodi ili wawapole pikipiki, kwa hiyo hapo kuweni makini na waangalifu sana,” alisema SP Zakaria.
MWISHO.


No comments:

Post a Comment